Wednesday, June 13, 2012

DMX haijui albam ya Jay-Z na Kanye West ‘Watch the Throne’



Kwa muda mrefu sasa DMX amesahaulika kwenye ulimwengu wa hip-hop na mbaya zaidi hajui nani ama ni nini 'Watch The Throne'!!

Kwenye interview na radio ya Philadelphia Hot 107.9 aliyofanya na DJ Q Deezy, DMX alifanya watu wagundue kuwa hakuwa na muda wa kutaka kuifahamu albam hiyo bora kabisa ya hip-pop ya Jay-Z na Kanye kwa mwaka jana.

Alipoulizwa kusema chochote kuhusiana na albam hiyo DMX alijibu: "What is that a TV show or something? What you call it? What’s it called again?"

Hiyo sio mara ya kwanza kwa emcee huyo wa Ruff Ryders kumtupia madongo  Hov tangu ajaribu kurudi kwenye game mwaka jana.

Kwenye interview na Power 105.1 February, X alimshutumu bosi huyo wa zamani wa Def Jam kuwa alisababisha makusudi kutoka kwa albam yake ya mwishi ili ‘kuondoa upinzani’.

No comments:

Post a Comment