Showing posts with label SPORTS. Show all posts
Showing posts with label SPORTS. Show all posts

Tuesday, July 10, 2012

Adam Nditi: Watanzania hata hawajali




Mchezaji mpya wa klabu ya Chelsea ya Uingereza kutoa Tanzania Adam Nditi ameibuka na kusema kuwa watanzania hawajali lolote.

Amesema wanachojali wao ni kupata jambo la kupigia soga pale wanakuwa wameboreka.
“All I can say Tanzania don't care at all, they care about is that the get something to talk about when they're bored,”ametweet leo.

Amesema hayo baada ya kuambiwa na mtanzania mmoja kwenye mtandao wa Twitter kuwa baadhi ya watanzania hawajashtuka na habari ya yeye kusajiliwa na Chelsea kwakuwa wamesikia kuwa amechukua uraia wa Uingereza.

“There are some doubts back in TZ. Just so you know. Some claim that you're only Tanzanian born but a legal UK citizen and not a Tanzanian, meaning you'll NEVER play for TZ. Any truth?” aliuliza mtu huyo aitwaye Givenality.

“Haha alright okay thanks for letting me know, am not saying anything about my personal life especially on twitter,” alijibu Nditi na kulikwepa swali hilo.


Sunday, July 8, 2012

Adam Nditi husikiliza Bongo Flava ili kupata mizuka!




Tangu kutangazwa habari kuwa mchezaji wa Tanzania (Zanzibar) Adam Nditi kusajiliwa na klabu ya Chelsea kama mchezaji wa kulipwa, mengi yameanza kujulikana kutoka kwake.

Nditi ambaye ni mtumiaji mzuri wa mtandao wa Twitter ameonesha kuwa pamoja na kukaa chini Uingereza tangu mwaka 2008, hajasahau muziki wa nyumbani.

Katika swali aliloulizwa na miongoni mwa watu wanaomfuata kwenye Twitter aliyetaka kujua ni kitu gani ambacho husikiliza kabla ya mechi ili kupata mzuka, alijibu husikiliza Bongo Flava.

Ni jambo zuri kuona bado anazifeel flava za nyumbani ambazo bila shaka humwongezea morali kwa kumkumbusha kuwa nyuma yake kuna watanzania kibao ambao si ndugu zake tu, wanaomwembea dua kila kukicha ili aendelea kufanikiwa zaidi.

Thursday, July 5, 2012

Adam Nditi achukuliwa na Chelsea kama mchezaji wa kulipwa



Mchezaji wa Tanzania Adam Nditi jana amesaini mkataba ‘rasmi’ kama mchezaji wa kulipwa wa klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza.

Kupitia Twitter jana ameandika; “Leo ni siku muhimu na ya kukumbuka kwangu na familia yangu na ningependa kumshukuru Mungu kwa kila kitu nilichonacho na vile navyokuwa.”

“Kuna wakati nakumbuka nilichoka kimwili na kiakili lakini baada masaa kadhaa ya mazoezi , kujituma na kufanya kazi kwa biddi naweza kusema hatimaye ndoto yangu imetimia.”

“I'd like to say well done to @Anditi3 for signing his pro contract with chelsea today! Official chelsea player! Well done bro! ‪#cfc” alipongezwa na miongoni mwa wachezaji aliokuwa nao Chelsea Academy aitwaye Dom Solanke.

”My bro @Anditi3 signed his professional contract with Chelsea FC, well done man.” aliandika mwingine.

"Thanks again everyone for saying all the good luck and only God knows what's ahead waiting for me," Nditi alitweet.

Adam alijiunga na Chelsea Academy mwaka 2008.

Alicheza kwa mara ya kwanza msimu wa 2010-11 dhidi ya Tottenham Hotspur.




Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya vijana ya Chelsea iliyoshinda kombe la FA mwaka 2011-12 na mara zote alikuwa akiingia kipindi cha kwanza isipokuwa kwenye mechi ya fainali dhidi ya Blackburn Rovers, ambapo aliingia kipindi cha pili.

Adam Nditi alizaliwa tarehe  18 September 1994 mjini  Zanzibar.

Hongera sana Adam.

Oklahoma City Thunder yamchukua Hasheem Thabeet



Timu ya Oklahoma City Thunder iliyoingia fainali mwaka huu kwenye ligi ya kikapu nchini Marekani NBA msimu ulioisha imekubali kuingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji wa Tanzania Hasheem Thabeet.


Thunder itakuwa ni timu ya nne kwa Thabeet, 25, tangu achukuliwe mwaka 2009 kwenye NBA Draft.


Mtanzania huyo mwenye urefu wa  7-foot-3 anashikilia rekodi hafifu ya wastani wa pointi 2.2 na rebounds 2.7 kwenye misimu mitatu akiwa na Memphis Grizzlies, Houston Rockets na Portland Trail Blazers.


Hata hivyo Thabeet atajikuta akikaa benchi mara nyingi kwakuwa Thunder, itawachukua pia wachezaji wakali kama Kendrick Perkins, Serge Ibaka, Nick Collison na Cole Aldrich msimu ujao.

Pia kwa mujibu wa makala ya mwandishi wa mtandao wa
kansascity.sbnation.com, Matt Conner amemponda Hasheem kwa makala yake ‘NBA Free Agency Rumors: Hasheem Thabeet To Thunder Should Not Excite Anyone’

Anasema, “Thabeet siku zote ameonesha kuwa zezeta mno ili kumruhusu kucheza dakika kadha kwa level za NBA.”

“Hiyo inamfanya Thabeet kuwa na mashaka kama atakuwa na muda wa kucheza akiwa na Oklahoma City Thunder.”

“Memphis Grizzlies huenda walifanya blunder kubwa zaidi kwenye historia ya NBA Draft kwa kumchukua Thabeet kama No. 2 mwaka 2009.”

Ameendelea kuandika, "na kwa utamaduni wa Thunder unaohusisha maendeleo na kukua, labda mwishowe Thabeet anaweza kugundua kipaji kidogo alichonacho.”

“He just hasn't had the kind of work ethic necessary to make it in the NBA.”




Tuesday, July 3, 2012

Wachezaji wanaounda timu ya kikapu ya US kwenye Olimpiki 2012

Lebron James  
Kobe Bryant
Carmelo Anthony
Tyson Chandler
Deron Williams
Chris Paul
Kevin Love
Kevin Durant
Russell Westbrook

Sam Saintfeit wa Ubelgiji kuwa kocha mpya wa Yanga




Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ethiopia mbelgiji Tom Saintfiet ana asilimia zaidi ya 90 ya kuwa kocha mpya wa Yanga.

Kocha huyo pia alikuwa ameomba kuifundisha timu ya taifa ya Kenya, lakini huenda akaja Yanga kwakuwa amepewa dau kubwa zaidi.

“He applied for the Kenya National Team job, but it would seem Yanga have offered him big bucks,” aliandika kocha mwenye leseni ya level B kutoka UEFA, Tom Legg.

Tom Saintfiet aliyezaliwa tarehe 29 March 1973 alianza kuwa kocha akiwa na miaka 24 na kumfanya kuwa manager mwenye umri mdogo zaidi kwenye soka la Ubelgiji.
 
Kiongozi wa usajili wa Yanga, Seif Ahmed alithibitisha kuwa kocha toka Ubelgiji, Tom Saintfiet ni miongoni mwa wawili wenye nafasi kubwa kutua Jangwani.

Timu alizozifundisha

1997-2001 -    Lower Belgian Divisions
2000       -     F.C. Satelitte Abidjan
2002-2003 -   B71 Sandur
2002-2003  -  Stormvogels Telstar
2003-2004 -   Al-Gharafa Sports Club
2004       -     Qatar U-17
2005-2006 -  BV Cloppenburg
2006-2007 -   FC Emmen (Technical Director)
2008       -     RoPS
2008-2010 -   Namibia
2010       -     Zimbabwe
2010-2011 -   Shabab Al-Ordon
2011       -      Ethiopia


Sunday, July 1, 2012

Watu milioni 250 duniani kote kumshuhudia Balotelli leo




Rekodi ya watazamaji milioni 250 duniani kote wanatarajiwa kuangalia fainali ya Euro kati ya Italia na Hispania itakayochezwa leo mjini Kiev. Idadi hiyo inadaiwa kuwa na hamu ya kumuona mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli akifanya mambo.


Idadi hiyo itajumuisha watu milioni 25 nchini Uingereza – idadi ambayo haijawahi kutokea katika historia ya kombe hilo na pia ni idadi ya tatu ya uangaliwaji wa mechi za soka kwenye TV.

“Hakuna shaka kuwa ‘Balotelli ni sababu’ iliyochangia kiasi kikubwa cha kuongezeka kwa watazamani.” Alisema mtaalam mmoja wa masuala ya TV.
“Sidhani kama watazamaji wanajua nini atafanya leo – na hiyo huvutia zaidi watazamaji.”

Idadi kubwa ya watazamaji wa mechi kwenye TV bado inaendelea kushikwa na mechi ya kombe la dunia mwaka 1966 wakati ambao Uingereza ilichukua kombe na kuangaliwa na watu milioni 32.5.

Bila shaka mshikaji wake Drizzy Drake ni miongoni mwa watu hao milioni 250 watakaomshudia Balotelli.


Wednesday, June 27, 2012

Roots of Fight - 'IRON' Mike Tyson Short Film





Roots of Fight is proud to honor the most devastating heavyweight boxer of all time, "Iron" Mike Tyson, with a new short film to commemorate Tyson's three victories in 1988, including his demolition of Michael Spinks on June 27th, that earned him the Undisputed Heavyweight Champion title, but also the rare "lineal" heavyweight championship of the world.

The stunning short film features Tyson and is anchored by boxing legend Ray "Boom Boom" Mancini, with insights from Randy Couture, Forrest Griffin, and Snoop Dogg.

To see the limited edition apparel and further exclusive content, visit http://www.rootsoffight.com

Monday, June 18, 2012

Didier Drogba kujiunga na klabu ya China (Shanghai Shenhua)



Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba anatarajiwa kusaini mkataba na timu ya Shanghai Shenhua, na kuungana na Nicolas Anelka kwenye klabu hiyo.

Mchezaji huyo raia wa Ivory Coast, 34, atatangaza uamuzi huo kwenye website yake binafsi.

Taarifa hizo zimetolewa na mwekezaji mkuu wa klabu hiyo Zhu Jun kwa shirika la habari la taifa la Xinhua.

Mkataba huo utamfanya Drogba alipwe paundi 200,000 ($314,000) kwa wiki.

Forward wa Ufaransa Anelka, aliyejiunga na Shenhua mwezi January naye akitokea Chelsea, aliwahi kuweka wazi kuwa angependa Drogba ajiunge na klabu hiyo ya kichina.

Hata hivyo Zhu amekanusha taarifa kuwa Drogba, aliyeondoka Chelsea baada ya kuisaidia klabu hiyo ya Ungereza kuchukua kombe la mabingwa wa ulaya mwezi uliopita kuwa atakuwa akilipwa, mshahara wa euro milioni 12 ($15.1 million).

Klabu hiyo tajiri ya Shenhua imekuwa ikitumia gharama kubwa kuwachukua wachezaji wa ulaya na makocha pia. Katika msimu huu wamemfukuza kocha Jean Tigana na kumleta kocha wa zamani wa Argentina Sergio Batista mwezi uliopita.

Kwa sasa timu hiyo inashikilia nafasi ya 12 kwenye ligi kuu ya China yenye timu 18.