Mama yake mzazi na msanii wa kizazi kipya nchini Tanzania Sunday Mangu aka Linex ameng’atwa na mbwa lakini katika juhudi za kumpatia matibabu, Linex amedai kuwa walikosa dawa ama sindano za kumchoma Mama yake katika mkoa mzima wa Kigoma ili kumwepusha na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Kutokana na hali hiyo Linex ambaye amewahi kutamba na ngoma kama 'Mama Halima' na 'Moyo Wenye Subira', amesema ilibidi wamsafirishe mama yake hadi jijini Mwanza kwa ajili ya kupata matibabu hayo.
“Hatimaye amemaliza dozi na yuko poa kafika jana Kigoma, ameandika Linex kwenye mtandao wa Facebook.
“Pamoja na kuwa Mama yangu amepona but still hiyo dawa na huduma nyingine muhimu ambazo hazipatikani, naomba wahusika waliangalie hilo kwa Mkoa ninaoupenda , ninaouwakilisha na nilipozaliwa”.

No comments:
Post a Comment