Wednesday, May 16, 2012

Jay-Z na Kanye West kuangusha party ya Tshs Bilioni 1.2 mjini London



Jay-Z na Kanye West wanatarajiwa kusherehekea show yao ya kwanza mjini London Uingereza kwa kuangusha party ya nguvu itakayogharimu paundi za Uingereza 500,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilionbi 1.2.

Maswahiiba hao wanaanza ziara yao ya barani Ulaya ijumaa hii mjini London pale O2 Arena, lakini watakula bata kwanza na kupop champagne za gharama wakiwa na watu wengine maarufu.

Kwa mujibu wa gazeti la Evening Standard, Jay na Kanye watakuwa wakila bata katika casino ya zamani iitwayo Fifty iliyopo St James's Street ambapo wataungana Beyonce pamojana mpenzi mpya wa Yeezy,  Kim Kardashian.

Karibu watu 400 wanatarajiwa kuhudhuria lakini unaambiwa meza moja inagharimu $1,000 mpaka £15,000.

"Hii ni kwajili ya kusherehekea usiku wa kwanza wa ziara yao ya barani Ulaya na wanataka London ijue kuwa wamewasili,” chanzo kimoja kimeliambia gazeti hilo.

"Sehemu hiyo itakuwa balaa sana na wanataka party hiyo iwe ya mwaka. Itakuwa imejaaa wanawake warembo na watu watakuwa wakipigania kuingia ndani”

No comments:

Post a Comment