Tuesday, May 15, 2012

Facebook yamkera Mo Racka aamua kupumzika kwa muda


Ni mara ngapi umeshawahi kuweka status Facebook na akaja 'mwehu' mmoja kusikojulikana na kucomment ujinga ambao ukaiharibu siku yako na mpaka ukatamani usirudi tena? 

Ni mara nyingi bila shaka. Ili kuwa mtumiaji mzuri wa mtandao huo wa kijamii huna budi kuwa mvumilivu kidogo.

Rapper Mo Racka ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki ameamua kupumzika kidogo na Facebook at least kwa kutoandika chochote baada ya kukerwa na jambo. Hata hivyo uamuzi huo haukuwa rahisi kutokana na jinsi mtandao huo wa kijamii ulivyo addictive.

"Usipokuwa na roho ngumu wallah humu facebook hutaondoka kamwe.

Yaani leo (May 7) nilikuwa nataka kujitoa humu facebook kuna mambo yalikuwa yamenikwaza, mh!! sasa katika kufuata process ndefu za kujitoa mwisho zikaanza kuja picha za rafiki zangu hapa facebook halafu wasichana warembo warembo, juu zimeandikwa majina yao mfano chausiku WILL MISS YOU, Alishaba will CRY, Tricia WILL REMAIN LONELY WITHOUT YOU, Tumtufye won't be happy without you.......
He!! kuona wale warembo na sura zao mbona nimeahirisha... .....ama kweli hapa kuna vi element vya u freemanson..hai wezekani” aliandika Mo.

May 8 mwaka huu akaandika “HII NI STATUS YANGU YA MWISHO YENYE UJUMBE MAALUMU KWAKO..

Maisha Ni PolePole, Ukipata Shida Leo Usilie...Wengi Wapo Kama Wewe Na Hawatoi Chozi...Usikae Chini Na Kulalamika Maisha Magumu...Usiwape Watu Nafasi Ya Kukucheka Na Kuwa Mfano Mbaya Kwa Wengine...Tazama Mifano Ya Waliofanikiwa Na Ufuate Njia Zao Utafanikiwa...Na Umuombe Mungu Akupe Uwezo...Unaweza , Jiamini!!!...Sitokuwepo kwa muda fb” alimalizia.

Angalau ameondoka Facebook kwa kuacha ujumbe mzito unaotupa picha kuwa sasa mtoto huyu wa kishua 'amekua'.

Hata hivyo ukitafuta jina lake Facebook utakuna na akaunti mbili za Mo Racka ambazo zote zina marafiki kibao. Hii ya pili hata hivyo kuna picha zake (hizo chini) alizoziweka May 11 kitu ambacho kinatupa maswali kuwa ameisusia moja na kuendelea na akaunti nyingine ya Facebook? 


No comments:

Post a Comment