Producer wa Tanzania aliyejizolea umaarufu hivi karibuni kwa midundo yake mikali Mesen Selekta, amepata mchongo wa maana kwa kushiriki kutengeneza ngoma kwenye mixtape ya Dj maarufu nchini Marekani, Dj Ill Will.
CV ya Dj huyo sio ndogo kwani ndiye Dj anayesimamia promo zote za nyimbo za YMCMB na ndiye aliyehost mixtape ya Chris Brown na Tyga “Fan of a Fan” iliyokuwa na hits kama Deuces na nyingine kibao.
![]() |
| Dj Ill Will akiwa na Tyga |
Dj Ill Will amemjulia wapi Mesen Selekta? Inasemekana kuwa msaidizi wake na Dj huyo alikutana na akaunti ya De Fatality ya mtandao wa Reverbnation na kupenda alichokisikia na kumwambia Dj Ill Will.
Muda huo Dj huyo alikuwa anaanda mixtape ya nyimbo nane na Dizzy Wright, hivyo akamtumia beat moja ili Mesen atafute wasanii watatu watakaoingiza sauti kwenye studio yake na mixing kufanyika Marekani.
Ndipo Mesen akamchukua P Bling, Fico na Goz B kuitemea mashairi beat hiyo. Lakini pia aliambiwa atume beat ambayo wasanii wa huko huko wakafanya ngoma iitwayo ROV.
Siku si nyingi P Bling, Fico na Goz B watakwea pipa hadi Marekani kwenda kufanya video ya ngoma yao iliyopo kwenye mixtape hiyo itakayoachiwa hivi karibuni.
Na baada ya mixtape hiyo iitwayo SmokeOut Conversations, Mesen Selekta amepewa kazi nyingi ya kuandaa beat matata kwa ajili ya Chris Brown.
Big up sana kwa Mesen Selekta kutokana na mafanikio hayo yanayoonesha namna mitandao ya kushare muziki kama Reverbnation ama Youtube ilivyo muhimu katika kutangaza kazi za wasanii na maproducer chipukizi. Pia kwa kuonesha kuwa Tanzania kuna vipaji vingi vinavyoweza kung'ara kimataifa.
Msikilize hapa P Bling kwenye beat iliyofanywa na Mesen Selekta ili upate jibu la kwanini Dj wa Kimarekani amependa kazi ya producer wa Tanzania.





No comments:
Post a Comment