Monday, May 14, 2012

Michelle Obama na Oprah Winfrey 'haziivi' tena


Wanawake wawili wenye asili ya Afrika na wenye umaarufu mkubwa Marekani,  Oprah Winfrey na  Michelle Obama, wanadaiwa kuwa hawaelewani na walishawahi kutukanana mbele za watu wao wa karibu, kwa mujibu wa kitabu kipya.

Kitabu hicho kilichopewa jina la The Amateur: Barack Obama in the White House,na kuandikwa na mhariri wa zamani wa New York Times Magazine Ed Klein, kimedai kuwa wanawake hao wamewahi kulumbana mara kadhaa behind the scenes,katika vita ambayo haikuwahi kujulikana kabla na baada ya  Barack Obama kuwa rais.

Kitabu hicho kimedai pia kuwa Michelle alimtuhumu Oprah kuwa anataka kutumia ikulu ya White House kuongeza utazamwaji wa show yake.

Kingine kilichoandikwa kwenye kitabu hicho ni kuwa Michelle aliwahi kuukejeli unene wa Oprah na kudai kuwa First Lady huyo anachukia watu wanene.


Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2008 ambapo Oprah alimuunga mkono Obama, muongozaji huyo wa talk show alikuwa karibu na Obama pamoja na mke wake.

Lakini mwandishi huyo wa kitabu hicho amesema kuwa baada ya uchaguzi kumalizika Michelle na wafanyakazi wake walimtenga Oprah.

Inadaiwa pia kuwa Rais Obama humpigia simu Oprah mara kwa mara usiku na kumuomba ushauri wa namna atakavyoongeza umaarufu, kitendo ambacho hakimfurahishi First Lady.

"Michelle anadhani Obama angemuuliza yeye na sio Oprah, ili kupata ushauri huo” kitabu hicho kimekinukuu chanzo ambacho hakikujitaja  jina.

Rais Obama alimwomba mke wake kumaliza ugomvi wao na Oprah, vyanzo vimekiambia kitabu hicho, na ndo maana Michelle alishiriki kwenye kipindi  cha Oprah May, 2011 kama show za mwisho mwisho za Oprah.

No comments:

Post a Comment