Hakuna kitu kinachomuumiza msanii kama akitoa wimbo ama video anayoamini kuwa ni kali lakini watu wanaichukulia poa.
Pamoja na kwamba video nyingi zinapigwa kwenye TV, siku hizi wasanii inawalazimu kuweka video zao YouTube ili kujitangaza zaidi nje ya mipaka.
Naziz ameamua kusema ya moyoni kuhusu watu kuchukulia poa video ya wimbo wake Afrika kwenye mtandao wa YouTube iliyowekwa tangu mwezi February mwaka huu.
Hadi leo hii video hiyo imeangaliwa mara 3,635, ina like 26 na dislike 1.
“It’s kind of depressing when u release a great video and people dont watch it.....” alitweet kwa kuambatanisha link ya video hiyo.
Africa ni wimbo wake mpya ambao video yake ilifanyika kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa ya 30 mwaka jana nyumbani kwao Lamu.

No comments:
Post a Comment