Tuesday, May 15, 2012

Prezzo amwomba msamaha Barbz


















 



 
Rapper kutoka Kenya Prezzo na mwakilishi wa Afrika Kusini Barbz katika jumba la Big Brother wameziacha tofauti zao na sasa wamekuwa marafiki. Hata hivyo urafiki huo haujaja kirahisi kwani wiki iliyopita waligombana kiasi ambacho wakawa hawasalimiani.

Kilichomuumiza zaidi Barbz ni kile kitendo cha kuambiwa kuwa umri wake umeenda sana na hana mume wala hana mtoto na kuwa hakuna mwanaume anayeweza kumuoa mwanamke mwenye miaka 35.

Maneno haya yalimuumiza sana Barbz kiasi cha kumfanya alie. Prezzo baadaye alikuja kuambiwa na Goldie kuwa maneno yake hayakuwa mazuri kwa mwanamke yeyote yule hivyo alitakiwa kumuomba msamaha na staa huyo mzee wa Bling Bling alikubali.

Kuomba huko kwa msamaha kwa Prezzo kulimfanya mrembo huyo wa Afrika Kusini kububujikwa na machozi kwakuwa hakutegemea kama Prezzo angenyenyekea baada ya kuwa amemkutakana kwa maneno makali.

Barbz alikubali kumsamehe Prezzo ambaye alimwambia kuwa kama angeweza kumnunulia maua ili kuprove kuwa alikuwa mkweli basi angefanya hivyo na wakakumbatiana huku Barbz akiendelea kububujikwa na machozi. 

Prezzo kuonesha uanaume akawa anambembeleza na kumkumbatia mrembo huyo. “Niamini wewe ni mrembo, pole, nchini kwetu huwa tunasema 'pole', hivyo nisamehe”alisema Prezzo na kumkumbatia tena kisha wote kwa pamoja wakacheka na kuondoka.
 
Baada ya hapo Barbz alionekana akiongea na akina dada wenzake mjengoni akiwaambia kuhusu Prezzo kumwomba msamaha.



Ni wazi kuwa Prezzo ametokea kujichukulia sifa kwa jinsi anavyoucheza mchezo ndani ya BBA ana nafasi nzuri ya kukaa kwa muda mrefu kama sio kuwa mshindi kabisa wa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment