Tuesday, May 15, 2012

Ligate: Never say wabongo hawasupport



Ni kama miezi miwili sasa tangu kampuni ya J&P Investments Inc. ya Marekani impeleke huko msanii wa kike kutoka THT, Linah Sanga.


CEO wa kampuni hiyo mtanzania Peter Ligate, amesema wakati wameanza kumpromote Linah nchini Marekani, msanii huyo alikuwa hajulikani kabisa huko.


Lakini kutokana na uwezo wake mzuri wa kutumia sauti yake stejini, kwa muda huo mfupi amegeuka kuwa mtu maarufu katika makundi ya watanzania na watu wengine kutoka Afrika Mashariki waishio Marekani, waliohudhuria show zake.


"Leo nasimama kwa kujivunia kusema kuwa zaidi ya watu 600 na idadi inaendelea kuongezeka, wamehudhuria show zake. Hii ni hatua kubwa kwake na kwenu ambao mmekuwa mkiacha maisha yenu ya ubusy na kuja kushow love. Never ever say wabongo hawasupport, huo utakuwa ni uongo" alisema Ligate.


Jumamosi hii Linah atakuwa akiperform huko Oakland Bay Area.

No comments:

Post a Comment