Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania na mwenyekiti mtendaji wa Bhitz Music Group Hermes Tyrol Lyimo maarufu kama Hermy B amewashauri wasanii wa muziki nchini hasa wanaochipukia kuachana na dhana kuwa muziki unalipa na wazingatie elimu.
Hermy B ambaye pia ni jaji wa mashindano ya kusaka vipaji vya uimbaji Afrika Mashariki ya Tusker Project Fame amesema wasanii wengi walioidharau elimu wakidhani muziki utawatoa kimaisha sasa hivi mambo ni magumu.
“Yaani wadogo zangu mnaohisi Bongo Fleva inalipa mmekosea sana na muangalie msije kuingia chaka”, aliandika Hermes katika ukurasa wake wa Facebook.
“Bora mkazie shule tu muwe na Plan B. Otherwise utakuja kujutia baadaye. Angalia wenzenu wanavyotabika”.
“Mimi shule imeniokoa sana ”alisema mhitimu huyo wa udaktari wa mifugo katika chuo cha SUA ambaye aliamua kwenda kusoma masuala ya muziki katika chuo cha The Recording Workshop.
Producer huyo anayesifika kwa kuwatengenezea hits wasanii kama AY na MwanaFA ameongeza kuwa hakuna msanii tajiri Tanzania .
“Honestly hakuna mwanamuziki wa Tanzania ambaye ni tajiri, tunadanganywa na images tu, anybody anaweza kuvaa vizuri, watuonyeshe vitu vya kweli to prove me wrong”
No comments:
Post a Comment