Wednesday, May 16, 2012

EXCLUSIVE: Pipi Doreen azungumzia Maisha, Muziki na Mapenzi






















Wiki hii mwanadada Pipi ameachia wimbo wake mpya uitwao “Unapokuwa Mbali” ambao umetengenezwa na Pancho Latino wa B’hits.

Kuna mengi usiyoyajua kuhusu mwanamuziki huyu aliyeawaacha wengi ‘Njia panda’ kutokana na utunzi wake uliogemea sana kwenye mapenzi.

Leotainment imezungumza naye ili kutaka kujua machache kati ya mengi yasiyojulikana kutoka kwa Pipi.

Leotainment:  Pipi ni jina lako kabisa?

Pipi:Hapana..naitwa Doreen Aurelian Cassian Ponera, na Pipi ilitokana na muigizaji Pipiro kutoka Nigeria ambaye wanafunzi wenzangu walinifananisha naye kwa utundu wangu wakati bado nipo school.

Leotainment: Kifo cha baba yako kilikuaffect vipi? Ulikuwa wapi wakati huo na ulikuwa unafanya nini?

Pipi:Baba yangu alifariki mwaka 2000 wakati nipo darasa la tatu na kabla ya kifo chake ni kama alijua akaniuliza nataka kusoma shule gani nzuri(kwa wakati huo) na nikamtajia but miezi saba baada ya kuanza kusoma shule hiyo (St. Marys) alifariki.

Alilazwa hospitali  kwa wakati huo watoto hatukuruhusiwa hospitali mpaka jumamosi. Lakini ni usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe nane mwezi wa saba ndo alifariki. Yaani nilisikitika japo nilikuwa mtoto kwani ni kama nilikosa kabisa kusema kwaheri..

Kifo chake kimeniaffect kwani naamini mtoto hukua vizuri kwa malezi ya pande zote mbili ingawa mama yangu ni sawa na baba kwangu pia.

Leotainment: Kwenye profile yako umeandika, “her mom was filling her with Celine Dion, Mariah Carey, Michael Bolton,Aretha Franklin, Michael Jackson and Luther Vandross..., Unamaanisha nini? Mama yako ana mchango gani kimuziki mpaka umefika hapo ulipo?

Pipi:Mama yangu ni mpenzi wa muziki tangu mi mdogo na bila yeye pengine muziki nisingeupenda kwani niliusikiliza most of the time....na hao wasanii ndo alikuwa anawapenda sana na akanirithisha na mimi pia.

Leotainment: Mwaka 2008 ulifika top 45 katika mashindano ya East African Pop idol, kama ungepata nafasi hiyo leo unadhani ungewakilisha vipi?

Pipi:  Mmmhhhh....kiukweli wakati naenda Pop Idol sikuwa hata najiamini na nililia machozi ya mshangao hivyo ningepata nafasi ya kusonga mbele na mashindano yale ningepata experience ya kutosha na confidence ambayo ingekuza personality yangu na labda kidogo Tanzania ingen'gaa kupitia mimi.

Leotainment: Umeandika kuwa unaweza kupiga piano na gitaa, ni kwa kiasi gani unaweza kuvitumia vifaa hivyo?
 
















Pipi: Nina ufahamu basic wa guitar na piano kwa msaada wa notation nilizojifunza chuo naweza kusema bado ni learner anayejitahidi.

Leotainment: Nyimbo zako nyingi tangu enzi za Njia Panda zina ujumbe wa kimapenzi zaidi, kwanini iko hivyo?

Pipi: Mapenzi..mapenzi..hahaha...hilo swali bana kila mtu anauliza...ni kwasababu ya upepo wa biashara lakini pia mimi nipo in love hivyo mapenzi yanani inspire kila siku katika uandishi.

Leotainment: Kitu gani usichokipenda katika mapenzi?

Pipi: Sipendi mtu anaye cheat...msimamo ni kitu muhimu sana.

Leotainment:Kama ungekuwa na uwezo wa kujiumbia mtu, ungependa kumtengeneza mume wako kwa mfano wa mtu gani? (jina)
Amini, Pipi na Barnaba



















Pipi: Hahaha!  ningemuumba huyu huyu niliye naye maana ananitosha na sijawahi kufikiria kama ningekuwa na wa aina nyingine!

Leotainment: Unauzungumziaje muziki wa sasa hivi? Mabaya na mazuri.

Pipi: Muziki sasa kuna ushindani mkubwa kwa wanaume japo nasikitika kwa wanawake tupo wachache lakini hata hivyo inahitajika elimu kwa wanaochipukia na hata waliopo kwenye game kuhusu kujitambua kwamba msanii ni ofisi na inahitaji wafanyakazi like management..n.k

Leotainment: Ni msanii gani wa kike wa Tanzania unatamani ufanye naye wimbo? Na wa kiume?

Pipi: Natamani kufanya collaboration na yoyote mwenye kipaji lakini tuwe na chemistry ya kuupendezesha huo wimbo...huwa nafikiria Shaa, Grace Matata na Damian Mihayo.

Shaa
Leotainment: Mwisho nini kimekufanya utoe UNAPOKUWA MBALI? Umemwandikia mtu?

Pipi: ‘Unapokuwa mbali’ originally ulikuwa wimbo wa Amini. Niliupenda na nikauomba lakini i took the chorus na part ya verse ya kwanza tu and the rest ni freestyle mwenyewe wakati nipo studio(B Hitz).Hivyo sikumuandikia mtu ingawa naweza sema composition yangu ilikuwa inspired na hisia zangu mwenyewe juu ya ninayempenda.

No comments:

Post a Comment