Friday, May 4, 2012

Wyre akusanya hela nyingi zaidi za upigwaji wa nyimbo redioni (royalties)

Wiki iliyopita chombo kinachosimamia haki miliki za wasanii nchini Kenya(Music Copyright Society of Kenya) kimetoa orodha ya wasanii wanaopata hela nyingi zaidi kutokana na malipo ya uchezwaji wa nyimbo katika radio (radio royalties)!

Msaani aliyejikusanyia cash ndefu zaidi ya kutunisha wallet yake alipata Kshs 491,718.83 sawa na Tshs 8,850,924.

Orodha ya wasanii waliopata pesa hizo ni pamoja na Wyre aliyepata airplay zaidi kutoka Radio Africa na Abbas Kubaff ambaye ngoma zake zilichezwa sana Capital FM.

Wengine ni Margaret Cheruiyot – Kass FM royalties, Betty Baiyo na Daddy Owen – Hope FM royalties, MOG – KTN royalties, Uko Flani Mau Mau – Ghetto Radio royalties.

Wengine ni Fadhili Williams – International Royalties, Safari Sounds – The Orchard Digital Distribution, St Joseph Catholic Church Choir Mbitini Parish – Liberty Afrika Royalties (Skiza tunes) na Joseph Wamumbe – Buni media royalties (XYZ Show).

MCSK inaendelea kukusanya data zingine za mirahaba na itawasilisha list nzima ya wale waliopata zaidi na kutatolewa tuzo Jumamosi ya 14th July 2012 katika hotel ya Hillton.

COSOTA inayosimamia haki miliki za wasanii nchini Tanzania imeshindwa kuvishawishi vituo vya radio kuanza kulipa mirahaba inayotokana na upigwaji wa nyimbo za wasanii mpaka sasa.

Kwa wanaoujua muziki wa Tanzania ulivyo sasa, wasanii wengi hasa wachanga hulazimika kuwapa hela madj na watangazaji ili nyimbo zao zipate promo zaidi! Unadhani Radio za Tanzania zinaweza kukubaliana na sharia hiyo?

Courtesy of This is creme.

No comments:

Post a Comment