Tuesday, May 15, 2012

Sababu ya Alicia Keys kumuita mwanae Misri (Egypt)


Siku chache kabla ya Mother’s Day Alicia Keys alihojiwa kwenye talk show iitwayo  ‘The Conversation’ inayotayarishwa na Demi Moore na mtangazaji akiwa Amanda de Cadenet.

Waliongea mengi kuhusu maisha yake kama mama, umbo lake baada ya kuzaa, kunyonyesha na sababu iliyomfanya amuite mwanae Misri.

“Well, Misri ilikuwa safari muhimu katika maisha yangu” Alisema Alicia. Ilikuja katika pointi ambayo nilikuwa nimefanya kazi mno bila kupumzika na sikuwa na idea yoyote kuhusu kuchukua likizo ya kweli na ilikuja katika muda huo ambao niliihitaji. 

Hivyo nilipoenda, ilinipa nguvu sana, ikanifungua macho, safari ya kihistoria, yenye nguvu na experience ya pekee iliyonifanya niipende Misri. 

Alicia, Demi na Amanda
Hivyo  ulipokuja wakati wa kumpa jina mtoto wetu, nililipenda, wote tulilipenda na tuliamua miezi kadhaa hata kabla hajazaliwa”
Egypt na baba yake Swizz Beatz
Kuhusu kwanini alienda peke yake nchini Misri alisema “Muda huo nilihitaji sana kwenda mbali  kiasi ambacho nilitaka kuwa peke yangu. Nadhani ni kitu muhimu kwasababu ukienda sehemu na watu lazima utakuwa ukifikiria kama wanafurahia ama wanapenda chakula unachopenda ama wanaufurahia mgahawa huu?

Nilikuwa nikisoma kitabu changu kwenye mgahawa na utaona mwanaume anakuja kwangu nakuuliza “Kuna mtu unangoja? Na mimi najibu kama “ Hapana, tuko hapa”. Ilikuwa safari yenye kusaidia sana”

No comments:

Post a Comment