Friday, May 4, 2012

Mastaa wa Tanzania na Baraza jipya la Mawaziri


Linapokuja suala la kutangazwa kwa Baraza jipya la mawaziri kila mmoja kuanzia mtu wa kawaida mpaka macelebrity wa Tanzania walikuwa na hamu ya kujua nani atakuwa nani! 


Baada ya kutangazwana na Rais Jakaya Kikwete majina ya mawaziri na manaibu wao , mjadala ukazuka kwenye mitandao ya kijamii, mtaani na kwingineko. 


Nyota wengi wa Tanzania hususan wanamuziki ambao huutumia sana mtandao wa Twitter kubadilishana mawazo, wameziweka wazi hisia zao kutokana na majina yaliyotangazwa. 

Katika mawaziri wote waliotangazwa, January Makamba ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technolojia ametia fora kwa kupongezwa zaidi na wasanii.


Ukweli uko wazi kuwa ujana wake na ukaribu na wasanii hao kwa namna fulani umewafanya wengi wamshangilie. Si wasanii tu waliompongeza kwa wingi Makamba bali pia wanasiasa wenzie vijana kama Zitto Kabwe na Halima Mdee.


Muda mfupi baadaye January aliwashukuru wote waliompongeza kwa kukamata shavu la unaibu waziri na kuwauliza ni mambo gani matatu katika sayansi na technolojia yanayowaathiri watu wa kawaida! (Sounds so responsible right?)




Mwingine aliyezikonga nyoyo za wasanii kwa kuchaguliwa kwake ni Amos Makala ambaye ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. 


Yeye (Makala) na waziri wake Dr. Fenella Mukangara watakuwa na mengi ya kuwafanya wakutane katika wakati fulani na wasanii hawa kutokana na wajibu wa wizara yao. 


Angalia Baraza Jipya la Mawaziri hapa

No comments:

Post a Comment