Wednesday, May 16, 2012

Kim Kardashian atamani awe rafiki wa Beyonce


Inasemekana kuwa Kim Kardashian anajaribu kufanya kila awezalo ili awe rafiki wa Beyonce.

Mrembo huyo mwenye miaka 31 anatamani mno kuwa na ukaribu na mwanamuziki huyo maarufu na mke wa Jay-Z na anaamini kuwa uhusiano wake na Kanye West unaweza kumsaidia kutimiza ndoto yake ya kuanzisha urafiki na mwimbaji huyo wa Halo.

Chanzo kimoja kimeliamnbia gazeti la New York Daily News kuwa,Kim atasherehekea siku akiwa pamoja na Beyonce na kupiga story kama marafiki. Kim ameamua kwenda mbali zaidi kwa  kujiandaa kumsindikiza mpenzi wake Kanye ili wakutane na Bey. 

Kanye na Jay-Z wanaanda tour ya albam yao 'Watch The Throne' barani Ulaya ambapo Beyonce atakuwa nao.

"Kim anataka kusafiri kila mahali na Kanye, lakini pia anajaribu kufanya lolote ili awe karibu na Beyonce," kilisema chanzo hicho.

Hivi karibu Kim amethibitisha kuwa Kanye ataonekana kwenye reality show ya familia hayo Kardashians ambapo imedaiwa kuwa Mama yake Kris Jenner amefurahia sana uamuzi huo.

"Sababu moja wapo ya kwanini Kris ameukubalia uhusiano wa Kim na Kanye ni kwasababu Kanye ana marafiki wengi mno maarifu” chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Hollywoodlife.com.


Kim na mama yake mwenye gauni jeusi wakiwa kwenye miongoni mwa video set ya show yao
''Kris anataka kumshawishi  Beyonce amemlete mwanae Blue Ivy na kumfanya aonekane kwa mara ya kwanza kwenye TV kupitia show yao. Anaamini kutakuwa na kipande kizuri sana pale Kim na Beyonce watakuwa wakiongea kuhusu watoto.

No comments:

Post a Comment