Tuesday, May 15, 2012

July Gichuru wa Citizen TV awa mtayarishaji wa filamu


Kama wewe ni mtazamaji mzuri wa Citizen TV ya Kenya jina na sura ya Julie Gichuru si vigeni kwako. 

Mwanamke huyu kiboko kwenye usomaji wa habari katika kituo hicho, ana vipaji vingi zaidi ya utangazaji.

Ameshaimba nyimbo kadhaa ukiwemo wa Jimmi Gaits ‘Furi Furi Dance’ akiwa na Bob “kutoka majuu” Collymore na Jeff Koinange. 
 
Sasa mtangazaji huyo msupuuu mrembo kutoka Kenya amejiingiza kwenye utengenezaji wa filamu na habari ni kuwa atakuwa mtayarishaji mkuu wa filamu iiitwayo Kimya.












Kuna taarifa pia kuwa ameshiriki kwenye production ya filamu zingine.

Kama akiamua kuigiza kabisa kwenye movie, tuna uhakika atafanya vizuri pia kutokana na kujiamini kwake na uzuri alionao.


No comments:

Post a Comment