Tuesday, May 15, 2012

Britney Spears na Demi Lovato wawa majaji wa The X Factor USA



Britney Spears na Demi Lovato wametangazwa rasmi kama majaji wa shindano la kuimba la The X Factor USA.

Baada ya miezi kadhaa ya fununu kuwa nani atamrithi Nicole Scherzinger na Paula Abdul, wawili hao walijumuika pamoja na majaji wenzao Simon Cowell na L.A. Reid katika tukio lilioandaliwa na kituo cha Fox jana mjini New York (14th May).

Akiongea kwenye tukio hilo Spears amesema :"Siwezi kuieleza furaha yangu kuchaguliwa kuwa jaji wa The X Factor. Ni shabiki mkubwa wa show hii na sasa napata nafasi ya kuwa sehemu ya show.  Simon na  L.A. ni bora wajiandae!"




















Lovato akaongeza: "Nimefurahi kujiunga na kundi la majaji wakongwe. Kuweza kuwa pamoja kila wiki na Simon, L.A. na Britney kutazama vipaji vya Marekani ni ndoto iliyotimia”

Kwa upande wake Simon alisema : "Nimejisikia raha sana kwa Britney na Demi kuungana nasi. Britney anabakia kuwa nyota mkubwa duniani, ana kipaji,anavutia na naamini anajua jinsi ya kutambua  The X Factor.”

“Demi amekuwa na career ya kuvutia kwenye muziki, TV na filamu kwa mtu mwenye umri kama wake. Ni mdogo, anajiamini na mchangamfu.Nadhani ni muhimu yeye kuzungumza na watazamaji wenye umri mdogo”



Britney anadaiwa kusaidi deal yenye thamani ya $15millionkwa kuwa jaji, jambo linalomfanya awe jaji wa kwenye TV anayelipwa zaidi tangu Jennifer Lopez asaini kuwa jaji wa American Idol.

No comments:

Post a Comment