Mambo yanazidi kuwanyookea Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square la nchini Nigeria.
Jana (May 31) wamesaini deal na miongoni mwa record label kubwa kabisa duniani, Universal Music Group.
Kupitia Twitter, Peter ameandika, “We r now ready 2 CHOP MORE MONEY now that we have gone UNIVERSAL..hehehehe!”
“Signed and sealed.... Psquare gone UNIVERSAL and the fans made it so possible. Thank u Lord,” aliongeza.
Kwa hatua hiyo kubwa waliyoifikia, Peter hakusahau kuwakumbuka mashabiki, “Thanks so much my beautiful pple, u all made it happen.... And may the good Lord bless us all.”
Shughuli hiyo imefanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Na sasa wamejiunga na label iliyo na wasanii zaidi ya 100 duniani. Miongoni mwa wasanii wakubwa waliochini ama waliowahi kuwa chini ya UMG ni pamoja na Young Jeezy, Wale, William, Tyga, Soulja Boy, Shania Twaim, Shantele, Steve Wonder, Akon, Rick Ross na Rihanna.
Wengine ni Nicki Minaj, Ne-yo, Nas, Melanie Fiona, Madonna, Lil Wayne, Keri Hilson, Kanye West, Justine Bieber, Jennifer Lopez, Drake, Dr. Dre na wengine wengi.
Makao makuu ya UMG yapo Santa Monica, California nchini Marekani lakini ina matawi yake sehemu mbalimbali duniani kote.