Sunday, August 19, 2012

J.Martins apaki Toyota Corolla, anunua Rolls Royce Phantom na Mercedes Benz G-Wagon



Baada ya kumiliki gari ya kawaida aina ya Toyota Corolla, producer na msanii wa Nigeria J Martins, ameamua kufumba macho na kununua mikoko miwili ya gharama za kuangusha shavu chini Rolls Royce Phantom na Mercedes Benz G-Wagon.
Rolls Royce Phantom (Makadirio ya bei yake dola 470,295)
G-Wagon ipo kwenye meli tayari ikipelekwa nchini Nigeria na masuala ya makaratasi yanachelewesha usafirishwaji wa Rolls Royce Phantom ambayo tayari ameshailipia.

Mercedes Benz G-Wagon (Makadirio ya bei yake dola 128,535)
Kwa sasa yupo nchini Marekani ambako anachukua kozi maalum ya masuala ya utayarishaji wa muziki jijini New York.

Akiongea na mtandao wa Showtime, aliweka wazi kuwa aliondoka Nigeria July 3 kwaajili ya kozi hiyo ya miezi mitatu.

Tayari ameshafanya video mbili kwenye majiji ya Miami na Los Angeles.

No comments:

Post a Comment