Monday, August 20, 2012

Zola D atandikwa KO round ya kwanza, mashuhuda wasema kaibiwa ushindi



Rapper na mwana masumbwi nchini Zola D leo amechezea kichapo kutoka kwa bondia Mchumia Tumbo baada ya kushindwa kwa Knock Out katika raundi ya kwanza.

Pambano hilo limefanyika jioni hii katika viwanja vya chuo cha bandari jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa shuhuda mmoja wa pambano hilo Zola D hajaangushwa na ngumi ya Mchumia Tumbo bali ulingo ulikuwa unateleza na mara kadhaa mabondia hao walikuwa wakianguka chini.

“Daah!!zola kashakaa unadhani bongo flava hii huyu mchumia tumbo hatari sana,” ameandika mmoja wa watu waliokuwa wakishuhudia pambano hilo.

“Kapigwa kibwege round ya 1 tu,” ameandika mwingine kupitia Facebook.

No comments:

Post a Comment