Sunday, August 19, 2012

Sony Music Africa: Albam mpya na video za Rose Muhando mbioni kutoka



Kampuni ya Sony Music Group kupitia label iliyo chini yake ya ROCKSTAR4000 imesema albam mpya ya Rose Muhando ipo kwenye utayarishaji wa mwisho mwisho ili iweze kutoka.

“In studio finishing album & music videos of 1 of Africa's biggest selling artists, Rose Muhando. Asante Sana! @SevenMos @SonyMusicAfrica,” ROCKSTAR4000 imeandika kupitiwa Twitter jumapili hii.

Hata hivyo haijasema albam hiyo inafanyika wapi japo wasanii wengi wa Sony Music Africa hurekodi nyimbo zao nchini Afrika Kusini.

Mwaka jana Rose Muhando alisaini mkataba wa kihistoria wa kurekodi albam tano na Sony Music Entertainment chini ya uongozi wa ROCKSTAR4000.

No comments:

Post a Comment