Friday, August 10, 2012

The Music Postmortem: Dogo Janja ft. PNC – Ya Moyoni




Dogo Janja ameachia wimbo na video ya kwanza tangu ajiunge na Mtanashati Entertainment. Ni ujio uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kutokana na tukio kubwa lilitokea miezi miwili iliyopita la msanii huyo kutoka Arusha kuzinguana na Madee kiasi cha Tip Top Connection kumrudisha Arusha.

Panel ya TMP inauchanachana wimbo huo kama ifuatavyo:

Josefly

Kweli nimeusikiliza vizuri sana huu wimbo wa Dogo Janja , tena zaidi ya mara kumi mfululizo na kwa awamu tofauti ili nijiridhishe kwa kile nitachokiandika hapa kwenye TMP, na hii nimeifanya kwa kujiuliza maswali na kutafakari sana kabla sijaandika lolote kwa sababu haya yaliyosemwa humu ni yaliyo moyoni mwa Dogo Janja.
Mbali na mdundo ulionishawishi kutikisa kichwa mara kwa mara, na hisia (feeling) za sauti nzuri ya PNC zinazosikika na kunitengenezea mood fulani, kiitikio kinachonipa sababu ya kupenda kusikiliza melody zake ,ni vizuri nizame kidogo kwenye mashairi na maudhui kama hivi:

Kwanza kabisa jina la wimbo na mashairi yanayosikika humo ndani vinaendana kwa asilimia 99.9 (YA MOYONI), kwa mtu anayefahamu tukio lililomtokea Dogo Janja na kundi alilotoka na kuhamia huko kwa watanashati wanaweza kukubaliana na mimi, hapa ukisiliza tu wimbo hata huhitaji mahojiano tena ili kuthibitisha kwa sababu jina la kundi/mtu ni kama ameli-mute hivi ila maneno yanajieleza wazi wazi.

Kwa kuwa wengi tulimsubiri kwa hamu kubwa Dogo Janja ataanza vipi huko kwa watanashati, alichokifanya yeye ni kujifaidisha kisanii kwa tukio ambalo watu wengi walilifuatilia ambalo lilimhusu yeye, naweza kusema Dogo Janja ameamua kufanya kile ambacho wengi(japo si wote) walitegemea kusikia kutoka kwake (ya moyoni mwake). kama muziki ni kuwakilisha hisia zako kwa jamii, basi dogo janja amefanya hivyo.

Mtunzi amejitahidi sana kutumia sanaa kufikisha ujumbe wake japo alikua anazungumzia yale aliyonayo moyoni ili yasichoshe sana, mfano angalia maneno haya..“Jasho langu kwenye shamba lao walifanya mbolea,…wakanifunga akili huku miguu inatembea” kwenye ubeti wa kwanza. Najua umepata tafsiri ya picha vizuri.

Nimejaribu pia kutafakari jinsi alivyorudia jina “Ustadh Juma na Musoma” mara ya kwanza niliona inakera kwenye kiitikio, lakini nimeijaribu kuunganisha tukio analozungumzia nikagundua kuna connection sana na huyu jamaa anayetajwa na kushukuriwa kwenye kiitikio cha wimbo na utanashat(kundi), japo hii desturi imekua ikiwakera watu wengi sana kwa kutaja majina ya managers na wawezeshaji kwenye nyimbo na hapo bado jina la producer, kundi la msanashati, washikaji wake na jina la msanii mwenyewe, ila imeshazoeleka nadhani ni moja ya mashariti ya wawezeshaji ili kujitangaza.

Changamoto; kwa mtazamo wangu huu ni wimbo ambao hautadumu saaana kimashairi kwenye akili ya  watu wengi, kwa sababu umeegemea sana kwenye tukio moja, hili tukio likizoeleka basi watu watauchukulia poa, labda itabaki melody tu na mdundo mzuri kuusogeza. Wapo watakaouchukulia kama ni wimbo wa majungu tu japo utampa mahojiano mengi na vyombo vya habari, lakini baada ya mwaka mmoja itakuaje, watauonaje? Dogo janja ajipange kutuonesha uwezo kwenye wimbo ujao kwa sababu huu utahit, pamoja na sababu nyingine, sababu kubwa sana ni tukio na misukosuko yake iliyohit sana kama topic za media.

Kinye

Binafsi nimependa wimbo unavyoanza…ladha nzuri ya PNC na beat nzuri ya Marco Chali.
YA MOYONI!! Kila mtu anajua wimbo huu umeelekezwa wapi…nasema kila mtu kwasababu issue ya Dogo ilizungumzwa kila kona mitaani na kwenye vyombo vya habari ndio usiseme, kiasi kwamba ikafika hatua wengi tulichoka kusikia kwani vilishazungumzwa vyote kwa undani. Kwa kusema hivi “vilishazungumzwa vyote kwa undani” niseme timing ya kuachiwa wimbo huu si muafaka hivyo nashawishika kwa kiasi kikubwa kusema kuwa wimbo huu hautakuwa gumzo kama nyingine za dogo zilizotangulia (japo sisemi huu ni wimbo mbaya), zaidi hautakuwa na maisha marefu.

JANJA!! Dogo ili uendelee ni vyema tusikupeleke kidogodogo, ni vyema ujue ukweli ili ufike mbali zaidi. Niseme tu utoto wako ndio uliofanya upokelewe vizuri, lakini utoto si kitu kinachodumu, kila leo mpya inayoingia mifupa yako inakomaa na sasa hivi ndevu zitaanza kukutoka hivyo kutoitwa mtoto tena…hii inamaana kuwa kila siku hakikisha unakua kifani, hapa najumuisha ukomavu wa mistari yako, ukomavu wa mtindo wako wa kuchana na vingine!! Nimebahatika kusikia wadogo wa aina yako kiumri, aisee wanaaandika na kuchana kuzidi hata ya wakubwa waliotoka, chukua tahadhari mapema na “UKAZE NANII”.

PNC!! Nimesikia matoleo yako kadhaa baada ya enzi ziiiile ukiwa “juu kwenye chati”…hapa tofauti ni kubwa sana, umesikika vizuri na niseme wazi kwamba chorus hii itakuweka pazuri…umeweka ladha nzuri sana na vionjo vya hatari!! Ingekuwa mimi ni wewe ningefikiria mara mbili kurudi kwenye production za aina hii na kuacha zile studio ulizoingia na kufanya nyimbo zako hivi karibuni.

MARCO CHALI!! Siyajui mahesabu na sayansi ya production hivyo nimuachie mtaalamu wetu. Lakini ni wazi sikio langu limeshasikia beats zako nyingi za namna hii na hakika limekaribia kuchoka. Upande wa mixing sina tatizo.

J-Ryder

Unaweza usiambiwe chochote na ukajua tu kwamba kwenye hii ngoma yupo Dogo Janja, Pnc na beat imetengenezwa na Marco Chali kutoka MJ Recs. Vionjo vinaongea vyenyewe.
Ujumbe na idea wa hii ngoma ni poa, ila Dogo Janja kama haja ongea ya moyoni haswa.
Vocals, mostly background vocals za Janjaro dah! verse nzima unaweza ukasikia anasema sema tu woww, wooww, wow! Oi, oii, oii! Be creative aisee.

Beat wise, naona hamna jipya and it lacks the dynamics, me nadhani Dogo Janja anahitaji something more big than this...of course its upon him and what he wants to achieve in his music career.

Mwishoni pale unasikia ile computer programmed Electric Guitar, kama sijakosea ni ile Slayer iliyopo kwenye Fruity Loops, naona ni producers (wengi) hapa Tanzania hawapendi (ama kwasababu hawana hio skill) ku-record live Electric Guitar/ Guitar inakuwa inashindikana.

Pia ina depend, kama producer mwenyewe hana skill yakuplay, you can simply hire an instrument player. In some cases Msanii/ Musician mwenyewe anajua ku-play instrument. The more Live it sounds, the better!

Kwa upande wangu PNC, alikuwa mkali enzi zile na Master J, ngoma zake kiukweli zilikua poa, sahivi design kama inakua ngumu kwake, ukiangalia kwamba kuna challenge za waimbaji wengine wengi wapya na wanaofanya vizuri.

Tusikilizie tu kitakachofuata toka kwa Dogo Janja 'cuz kwa sasa yupo na Mtanashati Ent. hope atafikisha malengo yake.

No comments:

Post a Comment