Saturday, August 18, 2012

Miraj Kikwete: Siasa si ajira ni wito



Mtoto mkubwa wa pili wa kiume wa Rais Jakaya Kikwete, Miraj mara nyingi amekuwa akiepuka kujihusisha na masuala ya kisiasa tofauti na kaka yake Ridhwan.

Pamoja na hivyo kuna wakati huutumia pia mtandao wa Facebook kuongea machache yanayogusa siasa.

Leo ameandika "kwa kweli inafurahisha kuona muamko wa vijana nchini katika siasa,kwa upande Mmoja ni jambo jema kujitambua na kutumia nafasi na haki zetu...ila jambo la kusikitisha wengi wetu tumekuwa ni wazandek na wanafki,wenye hurka za fujo na tamaa...SIASA SI AJIRA NI WITO".

Mwaka jana Miraj aliwaacha hoi marafiki zake kwenye mtandao huo baada ya kuweka picha mbili za viongozi wabunge na mawaziri,Wassira na Komba katika ukurasa wake wa Facebook wakiwa wamelala.

Kingine gazeti la Mtanzania Daima liliandika habari kuwa Miraj aliitetea CHADEMA kuwa ni chama cha Watanzania. Sounds like he loves the movement!

No comments:

Post a Comment