Saturday, August 18, 2012

Nape: mataifa ya nje yameweka vibaraka kuvuruga siasa ya Tanzania



Jumamosi katika kipindi cha Makutano ndani ya Magic FM katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye aliongea kuhusu kauli yake kuwa Harambee za CHADEMA ni za kisanii kwani kuna wafadhili ambao wako nje ya nchi wanaotumia mwanya huo kukifadhili chama hicho.

Mtangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akimkaribisha katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Nnauye kwenye studio za Magic FM
Nape alisema kuwa kuna hela chafu zinazoingizwa na Mataifa yanayotaka kuvuruga siasa na kuwaweka vibaraka ambao watafanya kile wanachotaka  watu hao wanaozimezea mate rasilimali za nchi husika huku akitolea mfano wa Congo.
Nape Nnauye katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango, Musa Kipanya na Mwanasheria Joseph alieelezea sheria za msajili wa vyama vya siasa.
Aliendelea kusema kuwa kuna pesa chafu ambazo zinaingizwa toka nje na kuchangiwa katika harambee na watu wanaojifanya ni wafanyabiashara wakubwa. Nape amewataka chadema kutoa majina ya watu waliowachangia na kazi wanazozifanya ili jamii iwatambue. 

Alipoulizwa kama anayafahamu majina ya wafadhili wa nje wa chadema kwa nini asiyataje Nape alijibu katika siasa kuna kitu kinaitwa “Timing” kwamba anasubiria wakati muafaka huku akitolea mfano wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alieitaka Serikali iwataje vigogo wanaomiliki mabilioni katika mabenki ya nje ya nchi la sivyo atawataja. 

Alimaliza kwa kutaka kila mtu ahakikishe anapigania amani ya nchi.

No comments:

Post a Comment