Sunday, August 19, 2012

Ujumbe wa Eid kutoka Leotainment



Tunayo furaha kuungana na waislam wote duniani katika sikukuu hii muhimu ya Eid El Fitr. Kwetu sisi tunaichukulia kama siku ya ushindi kwa waislam wote waliotumia siku 30 na ushee katika mfungo wa mwezi wa Ramadhan kwa kujinyima na kujitesa ili kukamilisha nguzo muhimu ya uislam. 

Tungependa kuchukua fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru waislam wote na wale wasio waislam kwa kutuunga mkono katika blog yetu. Pamoja na uchanga wake na ikiwa na miezi minne tu, Leotainment imekuwa miongoni wa blog zinazosomwa na wapenzi wa habari za burudani kwa wingi zaidi. 

Imekuwa chanzo cha habari kwa blog na website zingine nyingi ndani na nje kitu ambacho kamwe kisingewezekana pasipo ushirikiano kutoka wasomaji waaminifu wanaotuunga mkono siku zote. 

Ombi letu kwenu ni kuendelea kutuunga mkono bila kuchoka na pia kuwaambia marafiki na watu wa karibu kuhusu uwepo wetu. Tunaahidi kuendelea kuwa blog inayoandika habari za burudani kwa umakini na kuzingatia sheria zote za uandishi wa habari huku tukiendelea kukupasha kwa habari mpya muda wote.

Tunawatakia sikukuu njema yenye amani. Eid Mubarak.

Timu ya Leotainment.

No comments:

Post a Comment