Friday, August 10, 2012

New Music Video: G Nako ft. AY & The Artist - Take Off





Hongera kwa G Nako kwa kutake ‘risk’ kufanya ngoma na video hii. Ili kuweza kuelewa lengo lake la kuamua kufanya wimbo wa aina hii inabidi ufikirie ‘globally’ zaidi.Kwa maana kwamba hizi ni video ambazo ni rahisi kupata airplay kwenye vituo vikubwa vya runinga duniani hususan Channel O, Trace TV  na MTV Base ambazo zimetawaliwa na wanamuziki wa Nigeria na Afrika Kusini zaidi. 

Kwa wapenzi wa muziki wa Tanzania waliozoea kulishwa muziki wa aina moja wanaweza kusema G Nako amechemka lakini lahasha, hajachemka hata kidogo! He is on point. Hii video inaweza kuanzisha status mpya ya G Nako kama mwanamuziki wa kimataifa kwa maana ya kuanza kujulikana katika nyingi za Afrika kama ilivyo kwa AY na wasanii wengine wachache wa Tanzania.

Kuna taarifa kuwa label ya Sony Music Group Africa inataka kuwasaini wasanii kibao kutoka Afrika Mashariki na jana label iliyopo chini yake, ROCKSTAR4000 kupitia Twitter na Facebook iiliandika, “Another HOT HOT signing from East Africa to Sony Music Entertainment and ROCKSTAR4000... Who do you think it is??? (watch this space...)”. 

Kwa maana hiyo wasanii watakaopata mchongo huu kutoka Tanzania lazima waoneshe uwezo wa kuuzika kimataifa kama ilivyo kwa AY sasa hivi.

So big up kwa G Nako kulitambua hilo mapema.

No comments:

Post a Comment