Friday, August 17, 2012

The Music Postmortem: Profesa Jay ft. Dully Sykes – Hellow




Jumatano hii Profesa Jay ameachia ngoma mpya iitwayo Hellow. Producer ni Dully Sykes ambaye amefanya chorus. Hivi ndivyo panel ya TMP inauchambua wimbo huo.

Josefly

Hellow..kiujumla huu ni wimbo ambao unavuta usikivu hasa kwa majina haya..Dully Sykes + Professor Jay. Niliposikia hii collaboration nilipata hamu ya kutaka kusikia nini kimefanyika humu ndani.

Yap, huyu ndo Professor ninaemjua katika ngoma za party/club bang kama hizi, japo haikua bounce ila vijimambo nimeikumbuka hapa..na huyu ndiye Dully yule mwenye shangwe zake binafsi, sikiliza vinanda alivyopiga kwa mdomo japo kwenye chorus yuko serious.

Niligundua ili niandike vizuri hapa lazima niusikilize wimbo huu na kuwaza kama niko club halafu imepigwa hii ngoma, na hii ni kwa sababu ni direct for clubbing, japo tutaisikiliza na kuijudge mtaani…

Baada ya kuisikiliza vizuri niigundua kuwa hawa wasanii  wametumia uzoefu wao kuchagua nini cha kuimba kutokana na kila mmoja wao kumfahamu mwenzake kiundani. Ukisikiliza chorus aliyofanya Dully sykes imekaa vizuri  sana kwasababu wimbo inahamasisha wasikilizaji kurudisha feedback katika chorus hata kama hawataimba chorus yote lakini lazima watakua wanaitikia angalau hilo neno ‘HELLOW’.

Nimependa pia anavyoitikia hilo neno ‘hellow’ kwa kurelax tu japo beat inahamasisha sana. Kimashairi pia Professor Jay ameweza kutumia maneno fulani  mazuri, naweza kusema ameweza kucheza vizuri na maneno kwa kutumia sanaa vizuri kuyafikisha, kwa kuzingatia kuwa hii ngoma ni club bang maneno yaliyotumika yamekua direct kabisa kuwa ni kwaajili ya club, lakini ameyakandamizia  kwa kuweka misemo kadhaaa ya Kiswahili, mfano mwenye kisu kikali ndo daima hula nyama,na utunzi wake mwenyewe wa maneno mwanzoni tu mfano leo mambo yanajipa hata kwa beat ya mapipa…

Mbali na maneno yaliyotumiwa pia mtindo/style iliyotumiwa kurap iko poa kwa sababu amejaribu tu kuweka mtindo ambao kama  unaoimba wenyewe japo yeye anarap, hapa ukiusikiliza utapata hii sentensi, hebu sikiliza pale aliposema ‘nipe nikupe nikupe bila kero, juu kwa juu ruka kama yellow’ dakika ya ya1:04 hivi…

Hii ni hit kabisa, tena moja kwa moja kwa sababu beat ya kubounce imeshambulliwa vizuri na mashairi mazuri kiasi kwamba unaweza kuona kama huu wimbo ni mfupi sana wakati una verse 3. Kazi nzuri…hasa ukiupima kama uko club hivi halafu ukipigwa coz ndo mahala pake zaidi.

CHANGAMOTO: kuna neno professor kasema ‘amani kwa wanachoka wanatoka huyu anaingia’ imebaki kuwa ni tungo tata kwa watu wadadisi sana..je anamaanisha wanaotoka katika kundi la choka mbaya kisha wengine wanaingia? Au wanachoka wanaotoka club huku wengine wanaingia.. japo ni moja kati ya nyenzo ya kuwavuta zaidi watu wadadisi..na mara nyingine hii hutokea hata bila mtunzi kudhamiriaau kujua.

Kinye

Hellow!!!

Rahisi kufurahika hususani pale watu wanapokuwa wakicheza….ni kama Hi ya dully kipindi kile!!

Miondoko hii si migeni kwa Dully, na mkongwe kama Proffesor sidhani kama ilimuwia vigumu kuweka michano yake kwenye mdundo huu.
Nilichelewa kudownload huu wimbo, kabla hata sijausikia niliwaambia washkaji zangu kwamba ijumaa hii tutachambua Hellow ya Prof na Dully…wao walikuwa wameshausikia na wakacheka sana na kusema “kabla hata hujausikiliza andika tu kuwa ni mbaya” alisema mmoja na wote tukacheka.
Ni mtihani “kupostmotua” wimbo ambao tayari mtu wa kawaida tu aliye shabiki wa manguli hawa ameshaupondea.

Baada ya kuusikiliza.

Sioni kama ngoma hii ni mbaya…wala sisemi kwamba ngoma hii ni kiboko hasa kwa kuzingatia kuwa imefanywa na majamaa wenye heshima kubwa kwenye muziki wa Bongo.

Jay siku zote amekuwa makini kwenye kuachia nyimbo zake, kwa kuzingatia umakini na uwezo wake basi niseme kuwa hapa ameteleza.
Siku zote sizungumzi mengi kuhusiana na utengenezwaji wa wimbo, lakini sikio langu huwa linaweza kujua kisicho na ubora japo nakosa maelezo ya kitaalamu.

Hapa nisikiliza nyimbo tatu za Jay ninazozipenda sana na kiukweli zinasound vizuri kuliko hii.

Dully ni kama alikuwa na usongo sana…kama kawaida yake kelele zimekuwa nyingi kwenye wimbo…sijapenda anavyomaliza wimbo, haijasound poa.
Chorus hii haijawahi sikika lakini ukisikiliza kwa makini utagundua kuwa miondoko yake ni kama kionjo cha kwenye wimbo wa Dully kinachosema “jipindeee, kama wainama wainuka ipindeee”

J-Ryder

Autotune effect kwenye verse ya kwanza haijakaa poa, ukiimba off key sio rahisi ikubali siku zote...
Beat iko okay, ila kuna vitu kibao vya kurekebishwa...afu inaonekana kama imefanywa tu usiku fasta fasta, asubuhi ikaachiwa...haha labda...na hizi haraka za fiesta.

Pia ni kwamba inafanana na beats zingine alizowahi tengeneza...
Kingine ukisikiliza kwa makini sana..unaona sound ina compression/ limiter zaidi ama quality sio nzuri..

Na upande wa quality, sounds alizotumia mfano ikiwa ni Vst's, then iyo vst instrument yenyewe haikua recorded/ sampled properly...ndio maana sounds zinatofautiana, na pia ndio maana professional sound quality vst's cost thousands...simply 'cuz the technology used on the recorded instruments is up-to-date vinginevyo beats nyingi zina sound sawa kama they use kitu kile kile..

Chorus Dully alivyoimba nimeipenda...safi sana, background vocals za Dully kwenye verse za prof j sio kivile...na zingine zipo off key..
And most beats, unakuta wanapenda kutumia 'swing' fulani..ni freshii na inaleta groove..but naona inatumiwa sana hadi flavour yake ina fade away..

Vinginevyo, Prof. J ali-deserve beat kali zaidi ya hii, kwasababu ni msanii mkubwa na wa muda mrefu kwenye hii Music Industry ya Tanzania.



No comments:

Post a Comment