Good news ni kuwa Flavour wa Nigeria ana hit mpya sasa hivi aliyomshirikisha Fally Ipupa iitwayo Kwarikwa ambapo sehemu ya video hiyo ilifanyika nchini Ufaransa. Bad news ni kwamba ngoma hiyo amecopy kwa wasanii wa Ghana ambao sasa wanadai chao.
Wasanii hao wa kundi la Wutah wanadai Flavour ambaye jina lake halisi ni Chinedu Okoli ameiba utunzi wao.
Kwa mujibu wa vyanzo, wasanii hao Wutah Kobby na Wutah PV, wamesema hawajafurahishwa na tolea la wimbo huo uitwao 'Kwarikwa' ambao unafanana na ngoma yao iitwayo Kotosa.
Wanamshutumu Flavour kwa kuiba chorus, rhythm,mashairi na saxophone iliyopo kwenye beat hiyo na kwamba wao ndio wamiliki halali wa vionjo hivyo.
Kotosa ulitoka mwaka 2008 kabla ya kundi hilo kuvunjika mwaka 2010, na Kwarikwa ulitoka mwaka jana.
Hii si mara ya kwanza kwa Flavour kuiba vionjo vya wimbo mwingine kutoka nchini Ghana kwakuwa wimbo wake uliohit wa Nwa Baby ulikuwa na vionjo vya wimbo maarufu uitwao Ashawo uliokuwa maarufu nchini Ghana.
No comments:
Post a Comment