Monday, August 13, 2012

Fid Q kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kula viazi vitamu

Fid Q enzi za utoto
Siku zote Fareed Kubanda aka Fid ni mtu anayependa kuwa unique katika mambo yake. Leo ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa hapendi kusherehekea kama watu wengine walivyozoea kwa kuangusha party za gharama, kukata keki na kupop bottle kwa sana!

Kuonesha kwamba yeye ni ngoma halisi, Fid atasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kula viazi vitamu maarufu sana usukumani. Ukichanganya na maziwa ya mgando ama karanga zilizokaangwa, keki  haifui dafu! 

Fid ambaye siku yake ya kuzaliwa leo imemkuta kisiwani Ukerewe, ameiambia 255 ya XXL, Clouds FM kuwa amejisikia vibaya kukosa kituo cha yatima kujumuika na watoto katika siku yake hii muhimu.

No comments:

Post a Comment