Tuesday, July 17, 2012

Mtoto wa kufikia wa Usher bado hali ni mbaya



Mtoto wa kufikia wa Usher ambaye ni mtoto wa mke wake wa zamani Tameka Foster, Kile Glover anasemekana kuwa bado ana hali mbaya tangu apate ajali ya kugongwa na boti ziendazo kwa kasi wiki moja iliyopita.

Kile, alitangazwa kuwa ubongo wake umekufa siku chache tu baada ya kukimbizwa hospitali baada ya kugongwa kichwani na boti hiyo.

Mtoto huyo mwenye miaka 11 amewekwa hai na mashine maalum tangu ajali hiyo na vyanzo vimesema kuwa afya yake inazidi kuzorota.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa HollywoodLife kuwa muda wowote anaweza kufariki kwakuwa hali yake ni mbaya.

“Lakini hakuna mtu anayemuambia kitu Tameka kwasababu hafikirii kabisa kumuondelea mwanae mashine ya kumsaidia kuishi na bado anasubiria miujiza,” kilisema chanzo hicho.

Wakati ambapo Usher amekuwa akitembelea hospitalini hapo na kuwa pembeni ya kitanda alicholazwa Kile, watu walio karibu naye wamesema Usher anahofia kumwambia  Tameka kuwa akubali tu hakuna la kumsaiidia mtoto wake.

No comments:

Post a Comment