Friday, July 20, 2012

The Game aipiga chini harusi yake



Rapper wa West Coast,  The Game ameamua kuipiga chini harusi yake na mpenzi wake wa siku nyingi, Tiffany Cambridge.

Rapper huyo wa zamani wa G-Unit aliamua kuutumia mtandao wa Twitter kuthibitisha fununu hizo.

"Fununu hizo ni za kweli. Hakuna harusi tena. Sio kosa lake, ni langu. Ni mwanamke mzuri, sikuwa mwanaume wa kutosha kuliona hilo, alitweet jana July 19.

"Ujumbe muhimu kwa wanaume wote. Kama una bahati ya kuwa na mwanamke 1/2 ya niliyekuwa naye… mkubali na fanya chochote cha muhimu kumfanya awe na furaha.”

"I am truly sorry & apologetic to my family, friends & EVERYONE that this has affected & inconvenienced."

"Sio kila mtu huwa na mwisho wenye furaha.”

Maneno ya kutokuwepo kwa harusi hiyo yalianza mapema wiki hii.

Miezi tisa iliyopita, Game alikuwa anatarajia kumuoa Tiffney Cambridge July 28, na harusi yao kuoneshwa kwenye reality TV show ambayo ingeoneshwa kwenye kituo cha MTV..

"We regret to inform you that the wedding of Tiffney Cambridge & Jayceon Taylor has been cancelled," waliandika (MTV)

Tayari adui yake mkubwa  40 Glocc ameanza kumtupia maneno ya kejeli Game kutokana na hatua hiyo.

"D*MN.... I was about To make HeadLines, & Show up a that F*gget Wedding, & Give Him a Proper Dose Of the Real Sh*t Sh*t. ?#TheWeddingCrasher?," alitweet.

"I'm Still about To Yell, 'CHECK MATE!'." I was gone yell it at the @thegame WEDDING showin up in a tux to FIGHT but that's cancelled"

No comments:

Post a Comment