Sunday, July 22, 2012

Unafahamu kuwa Juliana Kanyomozi ni ‘binti mfalme wa Toro Kingdom?



Ukitaja wasanii wa kike wanaofanya vizuri nchini Uganda hukosi kuacha kulitaja jina la Juliana Kanyomozi. Wapenzi wa muziki Afrika Mashariki wanamfahamu zaidi kama jaji wa shindano la Tusker Project Fame. Lakini wengi hawafahamu kuwa mwimbaji huyu mrembo ni binti mfalme (Princess).

Akiongea na gazeti la The Star la Kenya, Juliana alisema kuwa yeye ni binamu wa kwanza wa Mfalme Oyo, Omukama of the House of Toro Kingdom.

Baba yake ambaye ni marehemu, na baba yake na Mfalme Oyo ni mtu na kaka yake, baba mmoja lakini mama tofauti.

Alipoulizwa lini mara ya mwisho alimuona Mfalme Oyo alisema, “Oh Nilionana naye miezi miwili iliyopita. Alikuwa nje ya nchi kwa masomo, lakini sasa amerejea.. Amekua sana.”

Katika mahojiano hayo pia Juliana alizungumzia pia uhusiano na baba wa mtoto wake wa kiume aitwaye Keron Kabugo.

Juliana na mchumba wake huyo wa zamani Amon Lukwago, waliishi pamoja kwa miaka sita kabla ya kuachana.

“Nilikuwa mpaka na pete ya uchumba lakini mambo hayakwenda sawa hivyo tuliamua kuachana,” alisema.

No comments:

Post a Comment