Friday, July 27, 2012

The Music Postmortem: Ngwair Ft. Mirror – Maskini Wenzangu


Wiki hii mwana Chamber Squad, Albert Mangwea ameachia ngoma yake mpya iitwayo 'Maskini Wenzangu' aliyomshirikisha Mirror. Producer wa ngoma hiyo ni Manecky wa AM RECORDS. Ijumaa ya leo panel ya TMP inauchana chana wimbo huo kuona mazuri na kasoro zake.

Josefly

Kama kawaida nitaegemea zaidi katika mashairi na utunzi kwa ujumla pamoja na jinsi ujumbe ulivyofikishwa kwa hadhira.
Kwa ufupi, Ngwair amefaulu katika utunzi, mpangilio wa matukio na mashairi. Idea kwa ujumla wake sio ngeni hasa ukizingatia kuwa kuna wasanii wengi tu wameshaimba kuhusu hali mbaya ya maisha ya watanzania na kilio kikubwa kikielekezwa kwa serikali. 
 
Lakini ubunifu alioutumia katika kuyaandika mashairi ya idea hii unaweza kuupa nafasi kubwa wimbo huu kueleweka vizuri na kuishinda ile hofu ya kwamba idea hii imezoeleka. Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi mtunzi alivyojitahidi kutumia sanaa ya ubunifu karibu kwenye kila mstari ambao ungeweza kuwa wa kawaida tu kama angeusema vile vile bila kutumia huu ubunifu. Mfano, ‘..Ndo maana wazanzibar wamechoka kutanga na nyika” hapo ujumbe kuhusu muungano..neno kutanga-na Nyika limetumiwa vizuri sana kuleta picha ya tatizo la muungano,…na maneno “big up Mandela leo South sio Africa” utaona neno South Africa lilivyotumika kusifia maendeleo ya South Africa.
 
Utunzi wa mtindo huu wa kucheza na maneno kama nilivyosema hapo juu unafanya verse ya kwanza kuwa fupi sana kwa kusikiliza. Pia mtunzi amefaulu kwa kiasi kikubwa kumfanya msikilizaji wa wimbo huu kuendelea kusikiliza zaidi kwa jinsi alivyoweza kupangilia na kumaliza na kitu kinachokuacha utafakari huku unasubiri ubeti wa pili… “leta mgomo baridi uijue serikali then muulize ULIMBOKA umuhimu wa madaktari. Hapa wengi watatafakari kwa sababu Ulimboka na swala la madaktari ni kitu ambacho kimeteka attention ya wengi Tanzania.
 
Hata katika ubeti wa pili na wa tatu ameendelea kucheza tu na maneno huku ujumbe ukiwa ni wa moja kwa moja (direct), mfano “tunaishi kiMungu-Mungu, toa M uweke Z upate kiZunguZungu”. 
 
Hapa msikilizaji pia atatafakari, na hapa atakua ameshirikishwa kuutafakari wimbo.akitoa M kwenye neno kiMunguMungu na akaweka Z.
Kila ubeti una maneno fUlani mazuri ya ubunifu tofauti na beti nyingine.

Naweza kusema kuWa huu mtindo alioutumia katika utunzi ndio umeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana kufikisha ujumbe wa moja kwa moja na unaweza kuuongezea muda wa kuishi katika masikio ya wasikilizaji, ukizingatia matukio aliyoyaweka ambayo mengi ni ya hivi karibuni.
Tone aliyoitumia ni ya kulalamika ambayo inaendana kabisa na idea ya wimbo, ‘Nalia na masikini wenzangu’. Mdundo(beat) ni mzuri sana kwa jinsi ulivyofiti kwenye wimbo, kazi nzuri AM records.
 
Changamoto; kwenye ubeti wa tatu kuna maneno kama wanafanya maongezi hivi., yale maneno yanavutia sana kuyasikiliza lakini neno la kwanza halieleweki vizuri..anaongelea babu wa loliondo anasema “hivi babu wa loliondo……kwa siasa, hayo maneno ya katikati yanachanganya,sijui nguli, nduli au ni nini..Kumbe anasema "'hivi babu wa Loliondo nae inawezekana tu ilikuwa ni siasa)!(Lakini iko wapi hii kaburi ya Balali !?"...
Ila kwa ujumla kazi ni nzuri ,kwa mtazamo wangu.
 
Kinye
 
Mwezi huu baadhi ya wana hiphop wamegusa mambo muhimu sana yanayotugusa moja kwa moja kwa namna tofauti…tazama Fid Q  alivyogusia issue nyeti ya mahusiano, Chidi Benzino naye akajivisha ubaya ufanywao na kila mtu na kuuwasilisha kwa hadhira, Msafiri Kondo naye akaamua kuianika nchi kwa namna yake ya kipekee tofauti kidooogo na Albert Magwea aliyeamua kuchana waziwazi yanayojiri nchini kwa kuanika na kuhoji.

Binafsi nilimmiss Ngwair…siku zote nimekuwa nikimpenda yeye wa namna hii…nikimaanisha yeye wa kuimba nyimbo zilizo serious sana “ni kwasababu tu kuwa anaziweza sana”...kwa waliopata bahati ya kuisikiliza a.k.a mimi watakuwa wanaungana name kuguswa na nyimbo kama sikiliza, zawadi, na a.k.a mimi ukiicha pembeni Jah Kaya ambayo ilitugawa mashabiki wake “si sana”
 
“Masikini Wenzangu”…title nzuri ambayo inamshawishi kila mmoja kutamani kusikia kilichoimbwa ndani. Hakika kila kilichoibwa ndani kimenifanya nilibariki jina la wimbo huu na si kufanya ubatizo wa jina jipya.
Mwanzo wa wimbo “zile 8Barz” ulinipa ushawishi wa kuendelea kuusikiliza wimbo huu japo sekunde ya 31 ilinikereketa sikioni baada ya sauti ya Mirror kuingia ikiwa haiendani na Key ya beat ktk sekunde ile ambayo mpishi aliibadilisha beat kwa namna yake aijuaye “mimi si mtaalamu” lakini najua alifanya kitu kwenye beat.
 
“Mirror”…simjui huyu jamaa lakini anaonekana kama sio mgeni kwenye mic. Ana sauti nzuri na kiukweli amepata melody nzuri kwa chorus ya wimbo huu…shida yangu kwake kwenye uumbaji wa mdomo wakati wa kutamka maneno…niseme tu kuwa mpaka wakati naandika hivi sijafanikiwa kusikia nini anatamka kwenye maneno ya kwanza ya mzungunguko wa pili wa chorus “kabla ya tunasuffer”
 
“Maneke”…producer bora wa mwaka kwa mujibu wa zile tuzo…honestly speaking hii si production ya kusadifu title yako…hujafanya kitu tusahau alivyosound Ngwair kwenye production za Bongo Records, KamaKawa, na Tongwe!!! Japo hii ni miongoni mwa beat nzuri sana za Hiphop ulizowahi kunyonga!
 
Kiujumla wimbo ni mzuri na kwa kiasi fulani utamfanya Ngwair aendelee kuwa na heshima ya kuwa Nguli wa huu muziki wa Bongo.

J-Ryder
 
Ngoma ukiiskiliza first time, huwezi kataa ni nzuri..na ujumbe unaeleweka freshii tu.
 
Ila tuingie ndani zaidi na tuone vitu vinavyoweza kurekebishwa.
 
Upande wa instrument alizotumia, asilimia nyingi zina interfere na frequency za vocals..hasa wa chorus...male vocals mara nyingi frequencies zinakaa roughly between 200hz to 2500hz, so cutting some from the brass would be good, also ina depend unataka emphasis iende upande upi..so kama ziende kwa vocals, then u cut from brass na other instruments ambazo zina require.
Pitch bend effect whIch is also called tape stop effect, on 1st verse, inahitaji marekebisho pia. Timing/speed yake me naona haipo sawa..unless thats the result they wanted.
 
Zile Rhodes (instrument) kama unavyoiskia throughout the song, ina interfere na bass...pia inahitaji tu cut freqs on the rhodes..mfano anything below 40hz can be cut, so to allow space for the bass...na pia bass unaweza cut below 20hz ama 30 hz, because the human ear inasikia between 20hz to 20khz...anything below or higher is usually unheard.
 
Pia kwa chorus, vocals zina ''sibilance'' (A sibilant speech sound, such as English (s), (sh), (z), or (zh)....na hii sibilance ni pale unaposikia herufi, ama neno kwenye vocals kama ''s'' ''ch'' ''sh'' ambazo zinakuwa loud. Njia za kupunguza hii kitu, either kurekebisha pale vocals zinapokuwa recorded, ama kutumia de-esser plugin, multiband compressor, volume automation, zote hizi zinaweza saidia kupunguza ukali wa hii sibilance.

No comments:

Post a Comment