Sunday, July 22, 2012

Obama huvaa ‘boxer’ za David Beckham



Gazeti la The Sun limebaini kuwa rais Barack Obama wa Marekani huvaa boxer za David Beckham.

Limesema Beckham alimtumia rais huyo boksi lenye karibu pair 50 za boxer zake baada ya kugundua kuwa Obama na mkewa Michelle ni mashabiki wakubwa wa boxer hizo.

Chanzo kimoja cha ikulu ya White House jana kimesema: “David aliahidi kutuma boksi la nguo hizo za ndani kwa rais na Michelle amesisitiza Obama azivae.

Pamoja na hivyo Becks, 37, anapendwa sana na watoto wa Obama Malia, 14, na Sasha, 11.

Wasichana hao ni mashabki wakubwa wa Becks kiasi cha kubandika picha zake kwenye kuta za vyumba vyao.

Chanzo hicho kimesema Beckham alikutana na familia hiyo alipoenda  Washington na waliangalia pamoja mechi ya kikapu jijini LA.

No comments:

Post a Comment