Sunday, July 22, 2012

Naeto C azawadiwa Porsche kama zawadi ya harusi



Weekend hii rapper wa Nigeria Naeto C amefunga ndoa na Nicole Chikwe.

Harusi yake ilihudhuriwa na watu maarufu na wazito nchini Nigeria akiwemo rais wa zamani wa Nigeria, Olusegen Obasanjo ambapo mama yake Naeto, Kema Chikwe alikuwa waziri wake.

Katika harusi hiyo wanandoa hao walizawadiwa gari mpya aina ya Porsche Cayenne yenye thamani ya Naira milioni 11 ambazo ni sawa na shilingi milioni 110.

Zawadi hiyo ilitolewa na mmiliki wa kampuni ya Auto Lounge, Larry Onuegbu.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa hiyo ilikuwa ni zawadi iliyotolewa na D’Banj ambaye ndiye aliyemkabidhi  hata hivyo.

No comments:

Post a Comment