Wednesday, July 25, 2012

What!!! Lisa Jensen ana watoto watatu?




Mwaka huu kwenye shindano la Miss World, Tanzania inawakilishwa na aliyekuwa mshindi wa tatu kwenye Miss Tanzania 2006 Lisa Jensen.
Shindano hilo litafanyika nchini China.

Katika video yake ya kujitambulisha iliyowekwa kwenye akaunti ya Youtube ya Miss World anasikika akisema, “I am raising three beautiful children back at home.” Ni sentesi ambayo imeanza kuleta mkanganyiko. 

“Did she say she is raising three children?” ni ujumbe ulioandikwa chini ya video hiyo na mtu aliyeiangalia.

Sentesi hiyo inaleta mkanganyiko kwakuwa haieleweki kama anaamaanisha analea watoto watatu wa kwake mwenyewe ama wadogo zake, ndugu zake, watoto yatima ama!!

Bila shaka itabidi atoe maelezo kufafanua kauli hiyo ili watu waujue ukweli.

No comments:

Post a Comment