Monday, July 23, 2012

Promoter adai Drake amegwaya kuzichapa na Chris Brown!



Mtandao wa Rumorfix umedai kuwa promoter wa masumbwi aliyekuwa ametoa ofa kwa Drake na Chris Brown waingie ulingoni kutwangana amesema Drake amegwaya!

Linapokuja suala la ngumi haijalishi mwaka wa kuzaliwa kwani Aubrey Drake Graham aliyezaliwa October 24, 1986 ni mkubwa zaidi ya Christopher Maurice Brown aliyezaliwa May 5, 1989.

Promoter huyo Damon Feldman amesema hakutakuwa na pambano hilo kwasababu Drake amefyata mkia kama mbwa aliyesikia sauti ya fisi!

Feldman na tajiri Alki David walitoa ofa ya dola milioni tano kwa wasanii hao ili wainge ulingoni kumaliza ubishi wao kwenye pambano la raundi tatu jijini Las Vegas.

Mwezi uliopita Chris alisema yupo tayari lakini Drake hawezi kuchukua uamuzi huo pengine labda kwa kuogopa kuabishwa.

Hata hivyo msemaji wa Breezy alisema kuwa bosi wake hakupewa ofa hiyo rasmi na Feldman ama  David na hata kama angepewa asingeshiriki kwenye pambano hilo.

No comments:

Post a Comment