Tuesday, July 17, 2012

J.LO akanusha kuwa alitaka aongezewe dola milioni 2 kwa American Idol.



Jennifer Lopez amezikanusha ripoti kuwa alipigwa chini na American Idol kwasababu alidai aongezewe malipo ya dola milioni 2.

Mwanamuziki huyo mrembo alitangaza wiki iliyopita kuwa anaacha kuwa jaji wa shindano hilo siku chache baada ya jaji mwenzie  Steve Tyler naye kusema anaipiga chini American Idol.

Ingawa J-Lo alithibitisha kuhusu kujitoa kama jaji wa American Idol kwenye interview na Ryan Seacrest kwamba ameamua kuondoka ili kuendelea na mambo yake mwenyewe, alikubali pia kuwa asingeweza kuendelea bila kuwepo Tyler.

"We had magic," Lopez aliiambia ABC News jumapili iliyopita.

"I don’t know, with him gone, it might be a different formula," nyota huyo aliongeza wakati akifanya concert yake ya Bell Centre mjini Montreal.

Katika hatua nyingine, mume wa Mariah Carey, Nick Cannon alizikanusha taarifa kuwa mke wake ataziba pengo la Jennifer kwenye show hiyo na kudai kuwa Mariah ni expensive mno!!


Hata hivyo mwanamuziki mkongwe Aretha Franklin, mshindi wa mara 18 wa tuzo za Grammy ambaye jarida la Rolling Stone lilimtaja kama ‘the greatest female singer of all time’, wiki iliyopita alikiambia kituo cha televisheni cha CNN kwa e-mail kuwa anapenda ajiunge na show hiyo kama jaji.

Franklin, 70, ni shabiki mkubwa wa show hiyo, na sasa badala ya kuingalia kwenye runinga kama wamarekani wengine, yuko tayari kuhusika katika kumchagua American Idol mpya.

Kuongezeka kwa Franklin kutasaidia kurudisha umaarufu wa “Idol,” ambayo ilipoteza nafasi ya kama show bora ya mwaka kwa kuzidiwa na kipindi cha NBC cha “Sunday Night Football.”

Kuwepo kwa mashindano mengine mapya ya aina hiyo yakiwemo The X Factor na The Voice kumefanya American Idol pia kupoteza watamazaji wengine.


No comments:

Post a Comment