Friday, July 20, 2012

Wateja wa mtandao wa Vodacom Tanzania watanufaika na ofa ya mwisho wa wiki



Wateja wa Vodacom Tanzania wana sababu ya kufurahi kipindi cha mwisho wa wiki kufuatia kuanzishwa kwa huduma mpya ambayo itawaruhusu kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi kwa gharama ya Shs. 250/- tu.

Huduma hii ni kwa mwisho wa wiki kuanzia Ijumaa saa 5 usiku hadi Jumatatu saa 1 asubuhi kwenda mitandao yote.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza huduma hii imekuja kufuatia kubaini kwamba watumiaji wa mtandao huu huhitaji huduma hizi kwa masaa mengi zaidi na wakati mwingine mpaka usiku mwingi.

"Tumekuja na huduma hii ili tuweze kuhakikisha kuwa tunawaridhisha wateja wetu na papo hapo wafurahi na wale wawapendao," alisema Meza.

Mkurugenzi mtendaji huyo aliongeza kuwa Mtandao wa Vodacom Tanzania unaona faraja kwa wateja na hivyo kuwa na hali ya kuwapa upendeleo mahsusi wateja wake ili kuongeza idadi ya watumiaji.

Huduma hii inakuja wiki moja baada ya kampuni hii kuzindua huduma nyingine inayowalenga vijana wa Kitanzania ambayo inatilia mkazo wa matumizi ya mitandao ya kijamii.

"Wateja wetu tayari wananufaika na matumizi ya bure ya mtandao wa kijamii wa facebook, twitter na wikepedia kupitia huduma ya "phoneson kwa wajanja". Pia tumeingia ubia na kampuni ya Nokia ili kuwawezesha vijana kupata huduma rahisi ya mtandao yaani Internet sambamba na mauzo ya bei ya chini ya simu aina ya ZTE ambazo zinauzwa hadi Shilingi 13,000/- yote hii ikiwa ni kutaka kuwapa raha wateja wetu," alimalizia Bwana Meza.

No comments:

Post a Comment