Sunday, July 22, 2012

Juacali aiokoa ndege dhidi ya ajali



Alipokuwa kwenye ziara yake barani Ulaya, mgenge Juacali aligeuka kuwa shujaa mjini Amsterdam, Uholanzi kwa kuizua ndege isipige mzinga kabla haijapaa.

Issue ilikuwa hivi: Juacali ndo kwanza alikuwa amepanda ndani ya ndege iliyokuwa inatoka Amsterdam kwenda London.

Alikuwa amepata siti ya dirishani. Alipochek nje aligundua kuwa injini ya kushoto ilikuwa inatoa moshi mweusi. Jamaa akagundua kuwa kuna tatizo.

Mara moja aliwataarifu wahudumu warembo wa ndege hiyo kuhusu tatizo hilo na baada ya muda mfupi kila mtu aliambia atoke nje ya ndege.

Marubani walikuwa waipaishe ndege hiyo bila kugundua tatizo hilo ambalo kama isingekuwa Juacali leo hii yangekuwa yanasemwa mengine.

Uongozi wa uwanja huo wa ndege uliilipia safari yake na wakampa tiketi kumi za bure za first class ambazo anaweza kuzitimia ndani ya miaka mitano.

No comments:

Post a Comment