Tuesday, July 31, 2012

Exclusive: Mtangazaji wa Ebony FM Iringa ampiga msanii wa Hip Hop

Man Kichefu

Kupitia ukurasa wa Facebook msanii wa hip hop wa mkoani Iringa Man Kichefu, leo ameandika, ‘jana nliitwa na eddo ebony.fm cha kushangaza alinivamia na kuanza kunipiga akidai nimemchafua! Poa mi sina noma ila nachoweza kusema its only the weak need to prove his strength through force! My mom hits more than anyone I ever met!”

Kufuatia status hiyo tumempigia simu Man Kichefu ili atueleze sababu ya yeye kupigwa na mtangazaji huyo.

“Kuna harakati fulani za muzki wa nyumbani hapa, unajue eeh, jamaa (Ebony Fm) wanatudiss sisi wasanii wa hapa. Kwahiyo kitu kilichokuja kufanyika kuna ngoma fulani sababu sisi kuna studio yetu tumefungua , tumejichanga tu mimi na mshikaji wangu tumefungua studio ,tumetengeza ngoma moja kwahiyo hiyo ngoma tuliyoitengeza inaitwa ‘Himaya ya Mkwawa’ inaelezea historia ya muziki wa Iringa na watu wa Iringa wale wanausuport muziki na wasio usupport. Baada ya ngoma hiyo niliiyoifanya sababu nimeiweka tu kwenye internet jamaa wakaichukua ile ngoma kitu kama wakaisikiliza hivi lakini mimi nikawa sijui.

Nikawa napewa tu taarifa kuwa jamaa anakutafuta kaongea sana redioni. Mwisho wa siku juzi akanipigia simu mimi nikaipokea tu kwa roho safi, ‘vipi  bro, fresh fresh’ akaniambia ebana na shida na wewe njoo ofisini.
Nikamwambia poa mimi nikaenda tu kwa roho safi. Ndio hivyo yanii nimeenda ofisini jamaa akaniita akaanza kunitukana pale anadai nimemchafua, kanivamia akaanza kunipiga.

Na baadhi ya wafanyakazi wengine yaani walikuja wakawa wananishika wananiambai ebana twende huku tukaongee. Pale ofisini kwao kuna sehemu moja nyuma ya ofisi kuna kibanda cha kupumzikia hivi, akaniita pale njoo tuongee.

Nimefika hapo ndo akaanza kunishambulia sasa mimi nikaona hili eneo si zuri sababu ni nyuma ya ofisi, nikakimbia nikaja nyuma ya ofisi.
Nimekuja mbele ya ofisi baadhi ya wafanyakazi wenzake wakaja wakanishika bana twende huku wakawa wananirudisha tena kule ambako jamaa alikuwa ananipiga yaani!
Eddo mtangazaji wa Ebony Fm
Kitu nilichokifanya mimi, nimefungua kesi polisi kwasababu ya ulinzi wangu wa mbele au kitu chochote kitakachoenda kule mbele lakini pia mimi sitaki nimfunge ama nimfanye lolote yaani.”

Tumemtafuta Eddo ili aeleze kwa upande wake lakini simu yake haipatikani.


Sikiliza interview yote hapa


Huu ndio wimbo wa Man Kichefu ulioleta mgogoro.

No comments:

Post a Comment