Thursday, July 26, 2012

Kristen Stewart wa Twilight Saga amcheat mpenzi wake Robert Pattson



Uhusiano wa miongoni mwa couple bora kabisa za Hollywood umeingia kwenye mgogoro mzito.

Ni Kristen Stewart na mpenzi wake wa miaka minne Robert Pattinson.


Kwa mujibu wa vyanzo ni kuwa Kristen ametembea na ditector wa filamu ya Snow White and the Huntsman Rupert Sanders.

Kutokana na tukio hilo Kristen Stewart ameandika barua ya kuomba radhi.
Muigizaji huyo wa filamu za Twilight alikamatwa akipigana busu na  Sanders mwenye mke na watoto wawili na kukubali kuwa amefanya kosa.

“Ninaomba msamaha kwa maumivu na fedheha niliyowasababishia wale walio karibu nami na kila mmoja aliyeathirika. Uzembe huu wa muda mfupi umehatarisha kitu muhimu zaidi katika maisha yangu, mtu nimpendaye zaidi na kumheshimu, Rob. I love him, I love him, I’m so sorry.”

Poor Rob!

Naye muongozaji huyo Rupert Sanders imembidi amuombe radhi mke wake kwa kumcheta na Kristen.


“Nimejisikia vibaya mno kwa maumivu niliyoipa familia yangu. Mke wangu mrembo na watoto wangu ndio vitu pekee nilivyonavyo kwenye dunia hii. I love them with all my heart. I am praying that we can get through this together.”

Kufuatia tukio baadhi ya watu maarufu nchini Marekani akiwemo Lady Gaga wamesema yao:"Geez this kirstew rob stuff is brutal. Makes me sad the way press acts. Hope they're ok (sic)."


Kazi wanayo!

No comments:

Post a Comment