Monday, July 30, 2012

Baada ya kucheat: Mashabiki waahidi kuzisusia filamu za Kristen Stewart wa Twilligt Saga



Mashabiki wa muigizaji Robert Pattinson wanatarajia kuzisusia filamu zote ambazo zitakuwa zimeigizwa na aliyekuwa mpenzi wake Kristen Stewart.

Muigizaji huyo wa kike anayeigiza kama Bella Swan kwenye filamu za series za 'Twilight' alikubali kumsaliti mpenzi wake Robert Pattinson kwa kuwa na uhusiano na muongozaji wa filamu ya 'Snow White And The Huntsman' Rupert Sanders.

Kitendo hicho tayari kimeanza kuathiri kazi za msichana huyo mrembo.

Rob na Kristen enzi za mahaba yao
Studio moja ya filamu imeliambia gazeti la The Sun: "Kristen ni mwanamke anayechukiwa zaidi Hollywood. Wapenzi wa filamu wa kike wamekuwa wakitafuta sababu ya kumchukia na sasa wameipata.

"Mashabiki wengi wa Rob' watazipotezea filamu zake. Itakuwa ni safari ndefu kurejea tena kikazi na kama mtu wa kawaida.”

Kutokana na tukio hilo Kristen na Robert waolikuwa wakiishi pamoja wametengana.

Hivi karibuni Rob alikuwa amepanga kumchumbia mpenzi wake huyo aliyeuvunja moyo wake kwa kuligawa penzi kwa mtu mwingine.

No comments:

Post a Comment