Monday, July 30, 2012

Alex wa BBA aandika barua kuelezea beef yake na Prezzo



Baada ya wakenya kumshambulia kwa kumuita sio mzalendo aliyekuwa mshiriki wa Kenya kwenye shindano la Big Brother Africa Stargame, Alex kutokana na kitendo chake cha kumtaja mkenya mwenzie Prezzo atolewe, ameamua kuandika barua kueleza kwanini alifanya hivyo.

"Hey fam, mambo mengi yamejitokeza tangu nimtaje mwananchi mwenzangu (Prezzo) kutolewa kwenye BBA Stargame 2012. Ningependa kutoa msimamo wangu kuhusiana na suala hili kwa matumaini tutakuwa na amani na kuendelea na maisha yetu.

Beef kubwa imekuwa ni kwamba eti mimi ni ‘msaliti’, sio mzalendo na si mpenda nchi yangu. Wakenya wenzangu, mimi si mtu wa aina hiyo.

Ninajivunia nchi yangu, naheshimu wananchi wenzangu na pia kuitangaza nchi yangu muda wote. Guys, nimekuzwa na uzalendo, utii na uamifu uliingizwa kwangu. Na ninaamini katika ubora huo. Ndio maana nimekuwa nikionesha bendera ya Kenya wakati wa show za eviction, wakati wa kazi na fursa zingine.

Sina haja ya kuwaambia hili lakini siku zote huwa nina bendera ya taifa langu chumbani. Sebule ya familia siku zote huwa na bendera juu ya sehemu ya moto (fire place). Gari ya familia yetu huwa na bendera ya Kenya muda wote – na niaimini nchi yangu kwa nguvu zote.

Kuna baadhi wanasema sikuweza kuimba wimbo wa taifa. Naiomba radhi nchi yangu kuwa nilikosea maneno ya mwisho ya wimbo wa taifa sababu ya kihoro (pressure). Lakini sababu ya uamifu wangu na imani juu ya nchi yangu nilirudia ubeti wote na kuimba bila makosa. Sikupenda kuingiza maneno yangu kujipatia ujiko. Naheshimu wimbo wa taifa wa nchi yangu.

Sasa swali limeendelea kuibuka kuhusu kumtaja mwenzangu kwenye  eviction. Jibu langu ni rahisi na la wazi: mwenzangu alikiuka interest zangu na uhuru wangu wa kujumuika (freedom of association). Uelewa wangu ni kwamba yeyote anayekiuka haki yako yeye ndiye sio mzalendo.

Mwenzangu alikuwa mbinafsi, alikuwa akificha vitu vya anasa mbali na washiriki wengine nikiwemo mimi. Pia alikuwa mkorofi kwangu. Alinizuia kutojumuika na Goldie, kwa kuniambia "You don't know me!". That's on record at BBA.

Napenda kusema kuwa yeyote atakaye chezea uhuru wangu na matwaka yangu halali, basi nina uhuru wa kuchukua uamuzi wangu wenye haki na niuonao wa muhimu kulinda matakwa na uhuru wangu.

Uchambuzi huo ulinifanya niamue kumtaja mwananchi mwenzangu.

Kwa kusema hayo, nakuheshimu, niheshimu na uzalendo huja baada ya mimi na wewe kutambua kuwa sote ni binadamu tulio na haki na uhuru sawa. 

Naipenda katiba mpya ya Kenya kwasababu ipo wazi kuhusu haki na uhuru wa wananchi.

Fam, ombi langu ni amani iendelee na tusonge mbele. Sina kinyongo na Prezzo na kama Africa ikiamua atakuwa mshindi, nitampongeza na kuwa na furaha kwaajili yake.

No comments:

Post a Comment