Kwa mujibu wa kituo cha ITV, meli ya Seagul iliyokuwa imebeba abiria 200 imezama kwenye kisiwa cha Chumbe visiwani Zanzibar.
Bado hakuna taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo lakini mwandishi wa ITV Zanzibar, Faruq Karim yupo na baadhi ya viongozi wakielekea kwenye eneo la tukio ili kujua mambo yakoje.
Haijujajulikana nini chanzo cha kuzama kwa meli hiyo lakini leo mamlaka ya hali ya hewa nchini ilitoa tahadhari ya kuwepo kwa kimbunga kikali kwenye bahari ya Hindi.
Zoezi la ukoaji halijaanza na meli hiyo imezama kwenye eneo lenye kina kirefu na kulikuwa na mawimbi makali na kwa sasa imegeuka juu chini!
Kwa mujibu wa mwandishi huyo hali ni mbaya.
Meli hiyo ya kampuni ya MV Seagul ilikuwa inatokea Dar kwenda Zanzibar.
Kuna taarifa kuwa kuna boti nyingine ilizama jana usiku kati Zanzibar na Pemba na watu wakaokolewa.
Mwaka jana zaidi ya watu 200 walipoteza maisha baada ya meli ya MV Spice Islander ilizama katika mkondo wa Nungwi Mkoa wa kaskazini ikielekea Pemba.
No comments:
Post a Comment