Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua ofa mpya kwa wateja wanaotumia huduma ya M-pesa kununua Luku ambapo sasa kila mteja atakae tumia huduma hiyo atapata muda wa bure wa maongezi wa shilingi elfu 1000 bila ya kujali ni mara ngapi mteja amenunua Luku kwa siku.
Muda huo wa maongezi ambao utadumu kwa siku mbili, mteja ataweza kuutumia kupiga simu kutoka Vodacom kwenda Vodacom na kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda mitandao yote Tanzania.
Huduma hiyo ya kununua Luku kupitia M – Pesa inawawezesha wateja mbalimbali kulipia na kununua umeme mjini na vijijini na kwa urahisi. Ili wateja kujua salio la muda huo wa bure wa maongezi, watahitajika kupiga *102# au *103#.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bwana Rene Meza, amesema kuwa ofa hiyo imelenga kuwahamasisha wateja wa Kampuni ya Vodacom kuendelea kutumia huduma ya M-pesa kununua Luku ikiwa ni njia ya kuendelea kuboresha huduma ya M-pesa sio tu kwa kutuma na kupokea pesa bali hata kuwawezesha wateja kufanya malipo mbalimbali kama kulipa ada za shule kupitia huduma hiyo.
“Ni kwa sababu hiyo ndio maana tunawapa motisha wateja wanaotumia huduma ya M-pesa kununua LUKU kwani tunataka waendelee kutumia huduma hii kadri wawezavyo na hata kuhamasisha wateja wote wa Vodacom kutumia huduma hiyo” alisema Meza huku akiongeza kuwa wale wote ambao hawajatumia huduma hiyo sasa wanayo sababu ya kuitumia.
“Huduma hii ni muafaka katika maisha ya sasa kwani inaokoa muda mwingi wa mazungumzo kwa wateja wetu. Napenda kuwapa changamoto wale ambao hawatumii huduma hii kuanza kuitumia kwani sasa tunaishi katika dunia ambayo ni muhimu kutunza muda” alisisitiza Meza.
Ofa hii imekuja punde tu baada ya kampuni hiyo kuzindua ofa nyingine mapema mwezi iliyotoa muda wa bure wa maongezi kwa wateja wanao tumia huduma ya M – Pesa kila wanapotuma na kupokea pesa.
Kwa mujibu wa Meza, kampuni ya Vodacom Tanzania inajivunia namna ambavyo wateja wake wanavyoiunga mkono katika huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo. Alisema kuwa Vodacom Tanzania inatambua mchango na thamani mkubwa waliopewa na wananchi ndio maana wanawapa huduma ambazo zinakidhi mahitaji yao ya kila siku.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 huduma ya M-pesa imeleta mabadiliko makubwa katika uhifadhi, utumaji, upokeaji wa pesa na manunuzi ya kila siku katika maeneo mbalimbali hapa nchini na sasa huduma hiyo inazaidi ya wateja milioni tatu nchini kote.

Kwa takribani miaka minne sasa huduma ya M-pesa imekuwa njia mbadala katika huduma za kifedha kwa wateja wa kampuni hiyo.
Huku jitihada za kuboresha na kuongeza matumizi ya huduma hiyo yakiongezeka siku hadi siku, Vodacom imefanikiwa kutengeneza mtandao wa mawakala zaidi ya elfu ishirini na tano na kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wateja wote nchini.
No comments:
Post a Comment