Monday, July 30, 2012

TMP Extra: Aman Joakim aionavyo ngoma mpya ya Ngwair



Amani Joakim ni mdogo wake na Hermy B. Kama kaka yake naye pia ni producer. Yeye pia alikubali kujiunga na jopo la wataalam wa muziki nchini wanaozifanyia uchambuzi nyimbo mpya za wasani wa Bongo. Bahati mbaya mchango wake tumeipata kwa kuchelewa na hivyo kutokana na umuhimu wake tumeamua kuuweka kwenye The Music Postmortem Extra. Hivi ndivyo aionavyo ngoma mpya ya Ngwair ft. Mirror - Maskini Wenzangu.



Nafikiri ni ngoma nzuri sana hasa kwa kipindi hichi cha wakati mgumu kwa mtanzania..kwa maana nyingine ni sauti ya mtanzania wa kawaida. Ni zile Ngoma ambazo zitapata Airplay kwa vipindi vya asubuhi kwa Radio.

Ngwea kama kawaida hajakosea chochote kitu. Flow kali japo sio kali kuliko zote alizowahi kufanya..mistari inaleta maana nzito lakini haichoshi kwani anatupia ladha za kiumaridadi wa kileo unapata hamu ya kuendelea kuskiliza mara kwa mara..

Nafikiri Kwenye maswala ya mdundo manecky amejitahidi pia lakini sio kazi yake bora, kwani nimewahi kuskia nyingine zilizo bora zaidi hata nyingine ambazo hazijatoka. Sidhani kama mdundo huu maneck aliumiza kichwa na wala sidhani alidhamiria kuumiza kichwa,ni ile midundo mikono inafanya tu na kiasi kidoogo cha utaalamu kutumika kwa hiyo sio kitu cha kumdahili ubora wake wa kutengeza mziki..ts an okay beat.

Mixing sio bora sana, vocals zina tatizo kiasi na hata mdundo wenyewe pia kwani mixing ya mdundo inategemea unataka kipi kisikike wapi,mda gani na kwa umbali gani. Labda kama alidhamiria iwe hivyo kwani siku hizi kuna standard nyiiingi saana za mixing kutokana na matakwa ya wasikilizaji wa mziki wa kileo ambao maskio yao yana mahitaji ya vitu vya ajabu kweli. 

USHAURI: kutokana na matatizo mengi sana kwa muziki wetu nafikiri mixing sio ishu sana,tutie mkazo sana kwa ubora wa midundo, uimbaji na uchukuajia sauti zilizo sawia..ukichukua sauti znazotakiwa hata ukishindwa kumix bado muziki unakua mzuri kwani tunapoimbiwa live hakuna mashine ya kumix ila ni sikio tupu na sauti halisi ya mwanamuziki.

No comments:

Post a Comment