Sunday, July 1, 2012

Watu milioni 250 duniani kote kumshuhudia Balotelli leo




Rekodi ya watazamaji milioni 250 duniani kote wanatarajiwa kuangalia fainali ya Euro kati ya Italia na Hispania itakayochezwa leo mjini Kiev. Idadi hiyo inadaiwa kuwa na hamu ya kumuona mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli akifanya mambo.


Idadi hiyo itajumuisha watu milioni 25 nchini Uingereza – idadi ambayo haijawahi kutokea katika historia ya kombe hilo na pia ni idadi ya tatu ya uangaliwaji wa mechi za soka kwenye TV.

“Hakuna shaka kuwa ‘Balotelli ni sababu’ iliyochangia kiasi kikubwa cha kuongezeka kwa watazamani.” Alisema mtaalam mmoja wa masuala ya TV.
“Sidhani kama watazamaji wanajua nini atafanya leo – na hiyo huvutia zaidi watazamaji.”

Idadi kubwa ya watazamaji wa mechi kwenye TV bado inaendelea kushikwa na mechi ya kombe la dunia mwaka 1966 wakati ambao Uingereza ilichukua kombe na kuangaliwa na watu milioni 32.5.

Bila shaka mshikaji wake Drizzy Drake ni miongoni mwa watu hao milioni 250 watakaomshudia Balotelli.


Fid Q kuachia video mpya kesho



Fareed Kubanda aka Fid Q kesho ataachia video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Sihitaji Marafiki’ aliomshirikisha mwanadada Yvonne.


Video hiyo imefanywa na kampuni ya Showbiz Defined iliyochini ya Mike T.

Huenda video hiyo inaweza kurudisha heshima ya kampuni ya Showbiz ambayo hivi karibuni ilikuwa kwenye vita kali kutokana na Mike T kutupiana maneno na director wake wa zamani, Eryne Epidu.

Ugomvi huo ulipelekea Epidu arudi kwao Uganda na kudai kuwa Mike T alimchomea kwa uhamiaji.

Naye Ngosha The Don mwishoni mwa mwezi uliopita alitangaza kuwa ile show yake ya online ya Fid Style Friday itaanza kuoneshwa rasmi kwenye TV za Afrika Mashariki mwezi huu.

Hayo yatakuwa ni mafanikio makubwa kwa rapper huyo mkali nchini kwakuwa show yake itaweza kuangaliwa na watu wengi zaidi.

Exclusive: Sikiliza track ya Breezy aliyomdiss Drake



Wakiwa wamepewa dau la $1 milli kila mmoja ili wapande stage kuzichapa live, Chris Brown na Drake wameendelea kutupiana mbovu kiasi ambacho kinazidi kuchochea zaidi beef lao.

Inaonekana ugomvi huu usiishe soon baada ya Chris Brown kumdiss Drake kwenye ngoma ya The Game iitwayo I don’t Like.

Kuna sehemu anasema “Wanarusha chupa, narusha mamodel sababu nampa Malaya pipe ndefu. Ntakuwa naimba, atakuwa anaimba, kwahiyo ni pambano, lakini subiri, simwoneshi mchizi taa ya kijani.”



“A fuck ni**a, that’s that shit I don’t like/ They throwin’ bottles, I’m throwin’ models just ’cause I give a bitch long pipe,” raps Breezy. “I be singin’, he be singin’, so it’s on, fight/ But hold up, I ain’t give a ni**a no green light/ This head up, my bread up, one on one, what you scared, bruh?/ Matter fact, take care bruh, you a pu**y ni**a/ My ni**a Tunechi, yeah that ni**a nice/ Shout out to Nicki, man, that ass tight/ Them eyebrows, man, them shits is yikes/ OVO, you overdosed, screamin’ YOLO no, I live twice.”

Kisikilize kipande chake hapa: