Rekodi ya watazamaji milioni 250 duniani kote wanatarajiwa kuangalia fainali ya Euro kati ya Italia na Hispania itakayochezwa leo mjini Kiev. Idadi hiyo inadaiwa kuwa na hamu ya kumuona mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli akifanya mambo.
Idadi hiyo itajumuisha watu milioni 25 nchini Uingereza – idadi ambayo haijawahi kutokea katika historia ya kombe hilo na pia ni idadi ya tatu ya uangaliwaji wa mechi za soka kwenye TV.
“Hakuna shaka kuwa ‘Balotelli ni sababu’ iliyochangia kiasi kikubwa cha kuongezeka kwa watazamani.” Alisema mtaalam mmoja wa masuala ya TV.
“Sidhani kama watazamaji wanajua nini atafanya leo – na hiyo huvutia zaidi watazamaji.”
Idadi kubwa ya watazamaji wa mechi kwenye TV bado inaendelea kushikwa na mechi ya kombe la dunia mwaka 1966 wakati ambao Uingereza ilichukua kombe na kuangaliwa na watu milioni 32.5.
Bila shaka mshikaji wake Drizzy Drake ni miongoni mwa watu hao milioni 250 watakaomshudia Balotelli.
No comments:
Post a Comment